Maumivu ya mifupa

Kichpox

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
361
Reaction score
397
Katika mada ya leo tatazungumzia baadhi ya matatizo au magonjwa yanayosababisha maumivu katika mifupa. Kwa sababu matatizo yanayoleta maumivu katika mifupa ni mengi mno, tutajaribu kuzungumzia yale tu amabayo huwapata watu wengi zaidi. Magonjwa ya mifupa hutokana na kukua kusiko kwa kawaida kwa mifupa au dosari yoyote ya msuguano. Dosari hizi huweza kusababisha mifupa isiwe na nguvu au maumivu katika maungio ya mifupa (joints). Upungufu wa madini ya calcium na vitamini D katika lishe au kuwa na uzito mkubwa husababisha kupungua uimara wa mifupa.


UZITO MKUBWA

Uzito unapokuwa mkubwa sana huadhiri magoti kuliko hata nyonga, kwa sababu uzito unapokuwa mkubwa magoti hubeba mzigo mkubwa na kufanya mifupa kusogeleana kutokana na kukutana kwa ute uliopo kwenye joints(maungio) ya goti na kusababisha mifupa laini kusagika na hatimaye kusababisha maumiv hii kitaalum inaitwa Osteoarthritis. Hii husababisha mtu kuwa na maumivu na hata kushindwa kutembea vizur
UMUHIMU WA VITAMINI D

Sababu nyingine inayopelekea maumivu ya mifupa ni ukosefu wa Vitamin D, japo hili huonekana zaidi kwa watoto lakini imekuwa chanzo kikuu cha maumivu ya mifupa.

Vitamini D ni miongoni mwa vitamini zinazochanganyika na mafuta. Nyingine katika kundi hili ni A,E na K. Vitamini D maarufu kama “vitamini ya jua” hujulikana kitaalamu pia kama (calciferol)(Ergocalciferol) Vitamini D3 (Cholecacliferol).

Vitamini D ni aina ambayo hupatikana katika aina chache za vyakula, lakini hupatikana pia kama virutubisho vya kutengeneza viwandani, au vyakula ambavyo huongezewa Vitamini D. Vyakula vyenye Vitamini D ni kama mayai, samaki, mafuta ya samaki, maziwa ya mama na maziwa ya wanyama. Mwili pia una uwezo wa kutengeneza vitamini hii na kujitosheleza kwa kupitia nishati ya jua. Kuota jua hasa nyakati za asubuhi huiwezesha miili yetu kutengeneza Vitamini D.

Vitamini hii inahitajika mwilini kwa ajili ya kurekebisha madini kalshamu (calcium) na phosphorasi (phosphorus) mwilini. Vitamini hii husaidi kusharabiwa mwilini kwa madini ya kalshamu na kuimarisha mifupa na meno. Kuota jua ni njia rahisi ya watu kujitengenezea vitamini D. Jua hasa la asubuhi linapokupata katika uso, mikono na miguu angalau mara 2 mpaka 4 kwa wiki itasababisha ngozi yako kutengeneza Vitamini D ya kutosha.



Baadhi ya magonjwa ya mifupa ambayo huwasumbua watu wengi zaidi ni:

Osteoporosis: Ugonjwa huu ni hali ambapo mifupa ya mtu inakosa viungo muhimu vya kuunda mifupa na kusababisha mifupa yake ikose uzito wa kutosha na kuifanya iwe myepesi kuvunjika. Mtu mwenye tatizo hili huweza kupungua urefu, huweza kupata maumivu makali na kubalilika katika ukaaji au utembeaji wake. Ugonjwa huu huweza kusababisha ulemavu wa kudumu.

Mtu hupata ugonjwa huu kutokana na kuzaliwa katika familia yenye historia ya ugonjwa huu kuwa amekoma hedhi na hasa anapokoma hedhi mapema mno kuwa mwanamke mwenye matatizo ya kupata siku zake matumizi ya madawa hasa yale ya kutibu asthma, matatizo ya thyroid n.k. kukosa madini ya kutosha ya aina ya calcium katika mlo kutokufanya mazoezi ya mwili kuvuta sigara kutumia pombe kwa wingi. Ugonjwa huu huendelea kukua taratibu bila kuonyesha dalili zo zote hadi mgonjwa atakapovunjika mfupa



Paget’s Disease:
Ugonjwa huu husababisha mifupa kukua na kuwa mikubwa kuliko kawaida. Mifupa hii huwa haina uimara. Mgonjwa huweza kupata maumivu na matatizo mengine ya kiafya.

Osteogenesis Imperfecta:
Huu ni ugonjwa wa kurithi ambapo mifupa ya mgonjwa huweza kuvunjika kiurahisi kabisa. Pamoja na kuwa na mifupa dhaifu mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri, kuwa na meno dhaifu na kupinda uti wa mgongo.

Bone Cancers:
Kansa ya mifupa inaweza ni ya kuanzia ndani ya mifupa au ile iliyoanzia katika viungo vingine vya mwili na kusambaa hadi kwenye mifupa, kwa mfano, kansa ya mapafu, kansa ya maziwa au kansa ya prostate. Kuna aina nyingi za kansa ambazo huanzia ndani ya mifupa kama leukemia, osteosarcoma, Ewing sarcoma, malignant fibrous histiocytoma na chondrosarcoma.

Rickets
Ni ugonjwa wa watoto ambao hudumaza ukuaji wa mtoto na huambatana na mifupa ambayo ni laini na dhaifu, mifupa ambayo haikujengeka vizuri, mtoto kuwa na uzito mdogo kulinganisha na umri pia kupinda kwa mifupa ambayo huzidiwa na uzito wa mwili (matege).Udhaifu wa mifupa hutokana na kutosharabiwa kwa madini ya kalshamu pia husababisha kushindwa kuziba kwa utosi wa mtoto(failure of the fontanelle to close).

Osteomalacia
Huu ni ugonjwa ambao huwapata watu wazima wenye upungufu wa Vitamini D. Ugonjwa huu hupelekea mifupa kuwa dhaifu,ambapo hupelekea kupinda kwa mifupa ya uti wa mgongo, udhaifu wa misuli, maumivu ya misuli na kupinda miguu kutokana na kuelemewa na uzito wa mwili. Vitamini D husaidia kusharabiwa kwa kalshamu kwenye damu na madini haya hupelekwa kwenye mifupa.Kwa hiyo pungufu wa vitamini hii hupelekea kalshamu iliyoko kwenye mifupa kwenda kwenye damu kwa ajili ya kazi nyingine za mwili kama utendaji kazi wa misuli.

Osteomyelitis: Osteomyelitis ni ugonjwa unaotokana na bacteria ambao hushambulia mifupa. Ni tatizo ambalo huweza kutokea ghafla au likawa la muda mrefu.

Arthritis
Kutokana na urefu wa makala hii ya arthritis, nitaelezea kidogo tuu hapa, makala nyingine utajifunza zaidi. Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yo yote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa cartilage inalika, upungufu wa synovial fluid, maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.



Kwa msaada zaidi ya tibalishe wasiliana
call/WhatsApp

0755932323
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…