Mama yangu anaumwa sana miguu na kiuno anapata maumivu makali sana. Alipimwa KCMC akaambiwa mifupa kwenye uti wa mgongo imelika ndiyo maana anapatwa na maumivu ya viungo na hakuna dawa ya kutibu ila tu atumie dawa za kutuliza maumivu. Nimeleta hata kwa kuwa kuna wataalamu wengi wa dawa haya za asili. Kama kuna anayefahamu dawa au ushauri wa nini kifanyike anisaidie bi mkubwa apone. Asanteni.