(1) Dawa ya maumivu ya Nyonga tumia Moja wapo wa hizi dawa inshallah kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu zitaweza kukusaidia.
Utwange Gramu 6 za mbegu za harmal achanganye na maji ya Uvuguvugu glasi moja awe anakunywa kutwa mara 3 kabla ya kula kitu kila siku kwa muda wa siku 12 inshallah atapona. kila akitumia afanye hivyo.
(2)Na ingine hii chemsha na maji Maganda ya limau kisha kuchemka awe anakunywa kutwa mara 3 glasi moja ya hayo maji kabla ya kula kitu Asubuhi,Mchana na usiku kwa muda wa siku 12 atapona inshallah.
(3) Na ingine hii Pata Asali safi mbichi ya nyuki changanya na unga wa mbegu za Harmal gram 5 awe anakunywa kutwa mara 3 Asubuhi kijiko kimoja cha kulia wali mchana kijiko kimoja na usiku kijiko kimoja kwa muda wa siku 12 atapona inshallah. awe anafanya hivyo kila wakati anapotumia hiyo dawa.
(4)Na hii ingine dawa ya kutibu hayo Maradhi ya nyonga Upate mafuta ya Hina uwe unamfanya masaji sehemu ile inayouma kwenye hiyo nyonga kila siku kutwa mara tatu kwa muda wa siku 12 inshallah atapona.
(5) au hii ya mwisho upate Mafuta ya lozi (mlozi) uwe unafanya masaji kama unavyo fanya kwa kutumia mafuta ya Hina inshallah atapona.
N.B Muhimu Dawa namba 1 Au dawa namba 3 unaweza kuchaguwa kutumia mojawapo kati ya hizo mbili sio kutumia zote 2 kwa wakati moja. Na zilizobakia waweza kutumia zote. Tumia kisha unipe Feedback.
Wakuu jana nilikuwa mazoezi nikicheza mpira wa miguu, nilijukuta nimepiga msamba na kupata maumivu makali yenye kunisababishia miguu ishindwe kunibeba juu ya paja (nyonga) mpaka sasa sijaweza kutoka kitandani! nikijaribu kupiga msamba naweza! ila maumivu yako juu ya paja linapoishia... kuna therapy yoyote ninayoweza kuitumia ili angalau inipe nafuu?...pls assist..
Habari wakuu nina maumivu makali sana ya nyonga upande wa kushoto hadi kunyanyua mguu ni shida sijui tatizo ni nini natanguliza shukurani zangu za dhati....
Pole sana.Nashauri nenda kapate kipimo hospital.Ukishidwa huko ntafute nitakwambia cha kufanya kwa na mimi nilisha kutwa na tatizo kama hilo siku za nyuma. ukinihitaji 0689 417472.
Mimi ni kijana wa miaka 34, nasumbuliwa na maumivu ya nyonga kuanzia katikati kuelekea upande wa kushoto nasikia kuna kitu kinachoma kuanzia kati kuelekea kushoto, kinachoma kama sindano halafu kinaacha.
Naomba msaada wa mawazo kama kuna mtu ameshakutana na tatizo kama hili au kama anamjua dokta au hospitali ambayo naweza pata matibabu kulingana na tatizo langu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.