Maumivu ya Nyonga na kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwa mwanamke...

Maumivu ya Nyonga na kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa kwa mwanamke...

Asha Hodhesh

Member
Joined
Mar 7, 2015
Posts
7
Reaction score
1
Doctor,

Mimi ni mama mwenye umri wa miaka 38 nimeolewa na nimejifungua mtoto wa kwanza nikiwa na umri wa miaka 29 na baada ya miaka saba nilijifungua mimba ya pili watoto wawili pacha.

Katika kipindi cha ujauzito nilianza kusumbuliwa na maumivu ya nyonga na mgongo hadi nikajifungua ile hali ikaendelea kwa kiasi cha miezi saba maumivu ya mgongo yakatoweka lakini maumivu ya nyonga yakaongezeka zaidi na kadri siku zinavyokwenda maumivu ya nyonga yanaisumbua sana.

Nilikwenda kumuona daktari alinishauri kutumia pain killer na mara moja nilichomwa sindano ya maumivu ya declofenac lakini maumivu yalitulia kwa siku 3 tu na hali bado iko vile vile.

Kingine ni kwamba tokea nimejifungua hadi sasa ni miezi 9 sijapata hedhi na sihisi kabisa hamu ya kujamiiana.

Naomba msaada wenu wa kitaalam please.
 
mmh pole dada, kwa hiyo mimba ya mapacha umejifungua ukiwa na miaka 36...... mmh sijui ni matokeo ya kubeba ujauzito ukiwa na umri mkubwa?? tusibiri wataalamu watufahamishe vizuri. maana me pia ni mgeni kwenye hayo mambo
 
aiseee babayangu pole ngoja wahusika wanakuja, ila nashauri ule vyakula vya kupandisha nyege usisahau karanga korosho na kadharika
 
Back
Top Bottom