Maumivu ya shingo na mgongo ofisini

Joined
May 15, 2019
Posts
69
Reaction score
23
HUTOKANA NA MIKAO MIBAYA/POOR POSTURE

Mara nyingi ukikaa muda mrefu kutumia computer huwa tunapata maumivu ya misuli ya shingo na mgongo.

Mikao mibaya husababisha tension kwenye misuli ya shingo (trapezius) na misuli ya mgongo(erector spinae)
pia husababisha mkandamizo mkubwa katika pingili za shingo na pingili za mgongo na kupelekea watu kupata matatizo ya disc eneo la shingo na mgongo ambao kwa kitaalam huitwa DISC BULGE

na matatizo mengine pia hutokea

Mfano
Cervical spondylosis

Lumbar spondylosis

Cervical myalgia (maumivu ya shingo)

Tension headache( kichwa kuuma mara kwa mara)

Muscle spasm(kukaza misuli ya shingo au mgongo)

picha chini[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116] zinaonyesha aina ya mikao mibaya na mizuri.

Na mikao hii huendena na mazingira yako ya kufanyia kazi kama
Aina ya kiti cha kukalia
Umbali kati ya kiti na dawati lako
Urefu wa meza/dawati
Umbali kati ya mikono na keyboard
Umbali wa monitor
Masaa ya kazi / mapumziko
Msongo wa kazi

Hivi vyote huchangia kutokea kwa matatizo hayo ya shingo.

Hivyo basi nakushauri urekebisha mazingira yako ya kazi kuendana na maelezo haya na mifano kwenye picha.

AU tafuta daktari wa Fiziotherapia awape elimu wafanyakazi wako kuhusiana na matatizo haya na namna za kujikinga.

kwa mawasiliano zaidi 0718 22 48 40
 
Hili ni tatizo kubwa sn kwasasa, migongo inawasumbuwa watu wengi mno, shida ni viti tunavyokalia haviko rafiki
 
Ahsante kwa elimu hii ya namna ya mikao salama na mibaya
 
kweli kabisa. viti sio rafiki. vipo viti sahihi vya kutumia. tunaita ergonomics chairs.

ukiachana na viti sisi wenyewe tunakaa masaa mengi kwenye kiti alaf tukiwa katika mkao mbaya.

pia na sababu hapo juu nilizo zitaja
Hili ni tatizo kubwa sn kwasasa, migongo inawasumbuwa watu wengi mno, shida ni viti tunavyokalia haviko rafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…