Huyu kocha kabla ya kuwa Napoli aliwahi kufundisha timu moja ya serie B kama sikosei ambapo ilifanya vizuri na baadaye akaonekana na Napoli ambayo wote tunajua jinsi walivyokua washindani wakubwa Juventus ambao wanaendelea kutawala serie A,Leo hii sarri yupo Chelsea,mpira unaochezwa pale unawafanya wachambuzi na wapenda soka wote walioinyima Chelsea nafasi ya ubingwa wameanza kuipa nafasi hiyo,Italia ina makocha bora sana miaka ya karibuni kama Roberto Mancini, Maurizio sarri,Carlo ancelloti,Gianfranco Zola,Antonia Conte,Massimiliano allegri na wengine wengi.