Maurizio Sarri na Sarrismo pale SSC Napoli, masterclass football

Maurizio Sarri na Sarrismo pale SSC Napoli, masterclass football

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Unalikumbuka lile chama la Naples, pale kwa watu wa soka nchini Italia? SSC Napoli ilikuwa hatari chini ya mfanyakazi wa benki ambaye pia ni mzaliwa wa Naples, Sarri.
.
Soka lake lilitambulika kama Sarrismo ila nchi ya Malkia Elizabeth namaanisha visiwa vya England wanaliita Sarriball, huyu bwana kwenye romantic football ni balaa[emoji119] soka lake lina tuvitu vitu kama kumtazama Shakira akiwa bafuni[emoji3]
.
Kulikuwa na starehe mbili pale Naples, ya kwanza ni yako, YES ile yako unayoijua [emoji23] kisha ya pili ni Sarrismo pale dimba la San Paolo, hizi ndio starehe zao rasmi
.
Sarri lile soka lake lilitaka vitu viwili, 'possession and progression' unamiliki mpira na kutembea kwenda mbele, Sarri hakuamini sana kwenye issue za kukaa na gozi la mnyama nyuma [emoji23]
.
Timu yake ilicheza sana 4-3-3, kwenye kujilinda ni 4-5-1 na kwenye attack ni 2-1-4-3[emoji119] marvelous with free flow football, Sarri alimwamini kila mchezaji wake kuwa ni ball player, hakutaka maguvu mengi kama Phil Jones[emoji3]
.
Anaekumbuka zile triangular passing za Napoli anyooshe kidole juu, anaemkumbuka Jorginho kama mboni ya falsafa hii afanye kama anajikuna, Jinho na Allan wale watoto wa Kibrazil waliswitch sana
.
Bila mpira walikuwa wanakabia juu, high line play wakiforce mpinzani apige backward passes au kufanya makosa, jamaa walikuwa kama mizimu [emoji119]
.
Nakumbuka pale kushoto Faouzi Ghoulam anatembea kwenye chaki ili akutane na Marek Hamsik, Insigne kisha wanampa gap Jose Callejon kuonesha ile 'Der raumdeuter role' mambo ya space finding haya [emoji3], transition ya kushambulia ilikuwa hivyo[emoji39]
.
Falsafa ya Sarri ilitubadilishia winger Dries Mertens kwenda straika baada ya kuondoka kwa Milki na Higuain, huyu Mertens kila mechi alikuwa kambani, hawa Napoli walikuwa wanangu sana hawa [emoji109]
.
Hai fatto un ottimo lavoro Allenatore Maurizio Sarri, pure Masterclass and Pure football Poet[emoji1756]
jr_farhanjr-20191201-0002.jpeg
 
Hahaha mkuu umetisha umemuelezea kwa umairi kwa sifa anazostahili.sasa aache mafegi aanze kupiga Cha chuga
 
Back
Top Bottom