BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
...kama ambavyo viongozi wote wanavyotakiwa kuorodhesha mali zao?
Date::12/4/2008
Kambi ya upinzani wahoji mabilioni ya Mramba, Yona
Na Salim Said
Mwananchi
SIKU chache baada ya mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, kutolewa gerezani kwa kuwasilisha hati za mali zenye thamani ya jumla ya Sh6.2 bilioni kama dhamana, wapinzani wameeleza kushtushwa na kiwango hicho cha mali kumilikiwa na watumishi wa serikali.
Hati za mali za Mramba, ambaye pamoja na Yona wameshtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi wakati wakiwa mawaziri, ni zile za nyumba yake na za washirika wake zenye thamani ya Sh3.14 bilioni, wakati hati za mali za Yona zilikuwa ni nyumba zake tatu zenye thamani ya jumla ya Sh3 bilioni.
Kiwango hicho cha thamani za mali kimewashtua wanasiasa wa upinzani.
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamehoji uhalali wa mtumishi wa umma kumiliki mali yenye thamani ya zaidi ya Sh3 bilioni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, viongozi wa Chadema na CUF walisema mshahara wa mtumishi wa umma unaeleweka.
Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jussa alisema ingawa dhamana ni haki yake, lakini Yona ameushangaza umma kumiliki mali yenye thamani hiyo ya fedha.
"Kimsingi, dhamana ni haki yao lakini tatizo linakuja pale mtumishi wa umma anapoweza kujidhamini mwenyewe kwa mali yenye thamani ya mabilioni ya shilingi," alionyesha mshangao Jussa.
Kwa mujibu wa Jussa, kitendo cha waziri huyo mstaafu kujidhamini kwa mali ya mabilioni hayo kinaweka maswali mengi dhidi ya viongozi wa serikali.
Jussa, ambaye ni mwanasheria kitaaluma, pia alihoji kasi ya kusikilizwa kwa rufaa yao wakati kuna watu wengi wamekata rufaa, lakini bado wanaendelea kusota rumande bila rufaa zao kusikilizwa haraka.
"Mimi, kama mwanasheria sioni tatizo la kupewa dhamana, lakini rufaa yao na ile ya serikali dhidi ya walimu inaibua maswali mengi ambayo majibu yake ni magumu kuhusiana na uhuru wa mahakama," alisisitiza Jussa.
Naye afisa habari wa Chadema, David Kafulila alisema haiwezekani kwa mtumishi wa umma kumiliki mali za namna hiyo.
"Hizo mali za Sh2.9 bilioni ni sehemu tu ya mali za Yona... kachomoa tu kidogo ili ziweze kumtoa nje, lakini alizipata kwa mshahara gani hata kama ni waziri," alihoji Kafulila.
Alisema mazingira kama hayo ya kutatanisha kwa kiongozi kumiliki mali za thamani hiyo, ndiyo yaliyovifanya vyama vya upinzani nchini kutaka uhakiki wa mali zote za viongozi wa serikali pamoja na akaunti zao za benki, lakini walikataliwa.
Kafulila alitoa mfano wa waziri wa zamani wa miundombinu, Andrew Chenge ambaye alijiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya ununuzi wa rada na kubainika kuwa ana akaunti yenye dola 1 milioni nje ya nchi, akisema ndilo lililojitokeza kwa mawaziri hao wawili.
"Kama mtu anaweza kumega sehemu tu ya mali yake yenye thamani ya 2.9 bilioni na kutoa kama dhamana mahakamani, kwa nini asiziite Sh.1 bilioni vijisenti," alihoji Kafulila.
"Tunataka uhakiki wa mali za viongozi wa serikali kufanyika ili kugundua madudu ya kifisadi," alisema Kafulila.
Aliongeza kwamba rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alitangaza mali zake wakati anaingia madarakani, lakini aliondoka kimyakimya huku Rais Jakaya Kikwete akingia kimyakimya pasipo kujulikana mali zake.