Naomba kuelimishwa, kwa mtazamo na ufahamu wangu ni kwamba Tanzania Football Federation (TFF) ni taasisi ambayo ina watendaji wenye ufahamu na weledi wa hali ya juu katika nyanja mbali mbali za kiutawala, fedha n.k. Siku ya Jumamosi na Jumapili ya wiki iliyopita nilipata fursa ya kwenda kuangalia ligi yetu ya Vodacom kati ya African Lyon na Toto Afrika na siku iliyofuata mechi kati ya Azam na Maji maji. Cha kushangaza taasisi kama TFF inatengeneza tiketi za mechi ya African Lyon na Toto Afrika na kuandika bei kwa maana ya kiingilio shilingi 5000/ lakini unatakiwa kulipa shilingi 7000/- kwasababu tiketi imegongwa muhuri kuonyesha ni shilingi 7000/- ! Hii inakuwaje, ina maana TFF haikufanya tathmini na kujua kwamba mechi ya Toto na Lyon inatakiwa kuwa shilingi 7000 ili waweze kutengeneza kabisa tiketi ambayo ni printed kwa bei hiyo ya shilingi 7000/ au ndio mjini shule? Cha kushangaza zaidi ni mechi ya Jumapili kati ya Azam na Majimaji, tiketi imeandikwa shilingi 5000/ bila huo muhuri wao wa 7000/ lakini watu tumelipa shilingi 7000/. Ukimuuliza muuzaji inakuwaje anakumbia kirahisi rahisi tu eti tumesahau kugonga muhuri ! Je mnataka tuamini kwamba TFF ni taasisi ya hovyo kiasi hicho kiasi kwamba wanashindwa hata kuandaa tiketi mpaka zigongwe mihuri. Je na vishina vya tiketi navyo vinagongwa huo muhuri kuonyesha kwamba zimeuzwa kwa shilingi 7000/- au ndo hizo shilingi 2000/ watu wanatia mifukoni? Ndugu Tenga unalijua hilo???????