Nikiingia mtandaoni nasoma kwamba Tanzania inauza nje ya nchi mazao ya kilimo kama vile mahindi, mchele, maharage, viazi n.k kwa matani na matani. Mtanisamehe kwa unyenyekevu wangu na uwazi wangu pengine na ujinga wangu pia.
Ila mauzo yanafanyikaje fanyikaje je watu binafsi kama vile wakulima wadogo wadogo, au ni mashirika makubwa na wafanyabiashara wakubwa wenye mashamba makubwa, au ni mashamba ya serikali? Na pia ni nani anayefanya hesabu kujumlisha pengine ni kiasi gani cha maharage kimeuzwa nje ya nchi?
Inaonekana kilimo ndio sekta yenye tija zaidi Tanzania, lakini kwa upande wangu nimezaliwa mjini, nimekulia mjini maisha yangu yalikuwa ni shule tu napenda sana hesabu. Ila mzunguko huu wa kibiashara wala sijauelewa. Tafadhalini watanzania wenzangu sisi sote ni ndugu naombeni mnieleweshe