Mauzo ya Sabasaba yashuka kutoka Tsh. Bilioni 7.06 mwaka 2025 hadi Tsh. Bilioni 3.9 mwaka 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yamewezesha kufanyika kwa mauzo ya papo kwa papo yenye thamani ya shilingi bilioni 3.9 huku zaidi ya asilimia 61 ya waoneshaji wakipata fursa za mauzo ya bidhaa nje ya nchi.
​
Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Dk. Latifa Mohamed Khamis, amesema hayo wakati wa kufungwa kwa maonesho hayo Julai 13, 2026 na kuongeza kuwa, mafanikio hayo yanaonyesha mchango wa maonesho hayo katika kukuza biashara, uwekezaji na kufungua masoko ya kimataifa kwa bidhaa za Tanzania.

Amesema zaidi ya nusu ya bidhaa zilizooneshwa katika maonesho hayo zilizalishwa nchini, hatua inayodhihirisha kuongezeka kwa uwezo wa uzalishaji wa ndani na ushindani wa bidhaa za Tanzania.

Kwa mujibu wa TANTRADE, zaidi ya wananchi elfu 97 walipata huduma mbalimbali za serikali na sekta binafsi kupitia vituo vya huduma vilivyokuwa ndani ya maonesho hayo.
Your browser is not able to display this video.

Mwaka 2026​

Kwenye Maonyesho ya 49, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliripoti ongezeko la asilimia 194 za mauzo ya papo kwa papo, kutoka Tsh. Bilioni 3.625 mwaka 2024, huku washiriki wakipata oda zenye thamani ya Tsh. Bilioni 44.87, na asilimia 70 wakifanikiwa kufikia malengo yao ya kupanua masoko na kukuza biashara zao.
Your browser is not able to display this video.

Mwaka 2025​
 
Na hizi bilioni tatu sio viingilio bali nni taasisi za Serilali zilizochukua vizimba na wafanyabiashara.

Walitoa malipo ya maji, umeme na Ulinzi(Matumizi) faida ikabaki milioni 200. Hawajasema tu
 
Si walisema wananchi walifurika! Hao wananchi walienda kushangaa tu hayo maonesho badala ya kununua bidhaa!
 
Mwaka Jana sabasaba na nilikuwa ndani ndani niliuza kama 12m

Mwaka huu nilikuwa eneo zuri Sana Sana nimeuza 4.6m

Yaani mwaka Jana Ile siku ya sabasaba niliuza kama 3m

Ila mwaka huu Ile siku ya sabasaba nimeuza 695k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…