Mauzo yanavutia lakini kwa faida ya laki 8 na matumizi laki 7 na elfu themanini nimehitimisha najitekenya, nimekubali kipigo till next time

Mauzo yanavutia lakini kwa faida ya laki 8 na matumizi laki 7 na elfu themanini nimehitimisha najitekenya, nimekubali kipigo till next time

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
A. Wastani wa faida kwa mwezi kwenye mauzo - 800,000

B. matumizi -

  • TRA (kwa mwaka) 300,000
  • leseni (kwa mwaka) 120,000
  • frem (laki 5 kwa mwezi) 6,000,000
  • Taka (elf 5 kila mwezi) 60,000
  • Mshahara wa binti (150,000 kila mwezi) 1,800,000
  • chakula na nauli (elf 3 kila siku kasoro j2) 954,000
  • vingine ( umeme, misiba, sabuni, n.k.) 200,000
  • gharama za kununua mzigo na usafiri zimeongezwa kwenye bei ya kujumua

  • Jumla 9,434,000 kwa mwake / 786,000 kwa mwezi

FAIDA YA MWEZI BAADA YA KUTOA MATUMIZI
A - B, 800,000 - 786,000 = 14.000
ELFU KUMI NA NNE


Maamuzi niliyoyachukua ni kufunga duka hasa ukizingatia nao mzigo umeisha, kwa sasa niendelee kutegemea kamshahara ka kodi za wananchi nijidundulize nirudi upya kivingine, maana kinachoendelea ni kujitenkenya.

pia soma:Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu
 
Kama ndo ivo hapo ulipaswa ufungue campun sio duka kwa biashara iyo iyo ili budget ya 600k irudi, hapo ulibid ulaze sio chini Mil30 ivi kwenye store zako kwamzunguk wa town ungewez kufanya izo return vzuri tu na kibunda chafaida kikabak
 
Kama ndo ivo hapo ulipaswa ufungue campun sio duka kwa biashara iyo iyo ili budget ya 600k irudi, hapo ulibid ulaze sio chini Mil30 ivi kwenye store zako kwamzunguk wa town ungewez kufanya izo return vzuri tu na kibunda chafaida kikabak
Kampuni corporate tax ni 30% si mchezo
 
Frame inakukaba,
Ukishajua wapi pesa zinavuja tafuta ufumbuzi sio kukimbia.

Nini cha kufanya.
Unatakiwa uangalie ni kwa namna gani unaweza kukuza mauzo, hapo ndio kazi kubwa ipo.

Kingine unapoanzisha biashara kama haijasimama mpaka kufikia kwenye peak, jitahidi kutotumia pesa unazoita faida kwa kipindi fulani ili biashara iendelee kukua na kujikuza zaidi.
 
Kampuni corporate tax ni 30% si mchezo
Ushauri aliotoa sio sahihi, biashara yako haina uhitaji wa kufanya hivyo, kwa mbeleni labda ukiangalia na ukuaji wake.

Kingine jitahidi kujifunza na kufuatilia mambo mbalimbali mfano hapo umeandika corporate tax 30% inaonesha dhahiri umeogopa kitu pasipo kuwa na taarifa sahihi.
 
Ukiijua siri ya biashara ya Kariakoo utawaheshimu na kuwaogopa wafanyabiashara wa hilo eneo.
Nimekuuliza vile kwa maksudi, umesema frame za kariakoo ni sawa na faida ya jamaa mara tatu,

Nilichokusudia kusema ni kwamba huwezi kulinganisha kariakoo na sehemu zingine, kariakoo ni soko na lango kuu kibiashara kwa maeneo yote na karibia biahsara zote Tanzania, hivyo basi mzunguko wa kibiashara kariakoo ni mkubwa ukilinganisha maeneo yote, hiyo pekee inaipa hadhi ya kuwa sehemu yenye thamani zaidi.
 
Kampuni corporate tax ni 30% si mchezo
Ila hapo ukipata wahasibu wazuri wa kukushauri mbona unachomoka, kuna mshikaj wangu ni general supply wa vitu vya ujenz na electionics aliwahi nionesha hesab zake kwa mwaka na interest za tra na wafanyakz ila bado anakunja faida ya maana tu sema mtaji alolaza ndio sio mchezo
 
Mkuu me naona changamoto kubwa hapo iko kwa binti, coz yeye umemuajiri, anafanya kazi kama muajiriwa, Biashara yoyote inahitaji commitment ya hali ya juu.... Watu wengi wanaofanya kazi wakianzisha biashara zinakufa,
Sababu kuu ni usimamizi mbovu, unaweza ukamuweka kijana dukani akawa haibi kabisa, ila changamoto ikawa ni namna anavofanya kazi

Hizi biashara ukiweka mabinti wengi wao wanaenda kuchat tuu na kusubiri wateja waje, hana wasiwasi hata, wala hana ubunifu wowote ule ili kuongeza mauzo,

Ukitaka kufanya biashara ingia frontline mwenyewe. Achana na Ajira yako uingie mazima hapo ndo utaweza kuona faida ya biashara
 
Apo ulitakiwa ufanye kupunguza matumizi....

Tra chezeshe tuwape 100.
Mfanyakazi mpe 200 afu ajitegemee mwenyewe....

Ungeongeza faida 170
Zaidi mwenyenyumba ungemchezesha pia wanaelewaga pia...
Ungeongeza matangazo ya biashara Yako baada ya mda flan ukemake profit mzuri zaidi
 
hapo tafuta zako fremu ya bei rahisi mazingira hayohayo, alafu chukua likizo hata ya mwezi kaa dukani mwenyewe uone changamoto na weakenss za kwenye biashara yako kisha ujue namna ya kuzisort alafu do online business fanya ku sponse ads ukiwa zako hukohuko ofisini we unadeal na wateja online tafuta namba ya ofisi we unakua nayo whatsapp dada anakua na line


biashara haitaki watu waoga
 
Back
Top Bottom