Mavazi ya waruga+ruga

Mavazi ya waruga+ruga

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Jeshi la waruga-ruga lilikuwa ni jeshi lililoundwa na mtemi Mirambo. Lilijumuisha watu aliowaokota huku na huko. Wangoni, watu waliokimbia utumwa, mateka wa kivita, na watu wengine waiosomeka.

Inasemwa kuwa mbinu kubwa ya jeshi hili ilikuwa ni kuwatisha adui zao. Walikuwa wakivaa vipande vyekundu vya nguo mabegani na kuwaambia maadui zao, "damu yenu hii."

Kichwani walivaa kofia zilizotengenezwa kwa mafuvu ya watu. Shingoni walivaa mkufu uliotengenezwa kwa meno ya watu. Ma kiunoni walijifunga mkanda uliotokana na utumbo wa watu.
 
Tuwekee kapicha hata ka mrugaruga mmoja tu tumuone anavyotisha.
watu wa zamani muda mwingine ilikuwa kama hamnazo mambo yao. Sasa mtu kajiwekea kakitambaa kekundu begani anakutisha eti "damu yako hii"
Ukiogopa hapo si uzuzu tayari
 
😀😀Hahaaa, lakini hapo ana fuvu la mtu kichwani, meno ya mtu shingoni na utumbo wa mtu kiunoni.
 
Stori za darasa la 3b, huo muda mko vitani anakutisha vp na icho kitambaa kwamba ni damu
 
Unaambiwa njia ya kuingilia ikulu ya Mirambo ilikuwa imepangwa mafuvu ya watu huku na huku. Kama wato wanavyopanga mawe au matofali pembeni ya njia.😀😀
 
Jeshi la waruga-ruga lilikuwa ni jeshi lililoundwa na mtemi Mirambo. Lilijumuisha watu aliowaokota huku na huko. Wangoni, watu waliokimbia utumwa, mateka wa kivita, na watu wengine waiosomeka.

Inasemwa kuwa mbinu kubwa ya jeshi hili ilikuwa ni kuwatisha adui zao. Walikuwa wakivaa vipande vyekundu vya nguo mabegani na kuwaambia maadui zao, "damu yenu hii."

Kichwani walivaa kofia zilizotengenezwa kwa mafuvu ya watu. Shingoni walivaa mkufu uliotengenezwa kwa meno ya watu. Ma kiunoni walijifunga mkanda uliotokana na utumbo wa watu.
Weka chanzo cha taarifa au utuambie ulikuwepo enzi hizo
 
Piga sana nyama choma na jamaa zangu, Mirambo, man Hamed bin Muhammed El Murjebi; nyie mnamwitaga Tippu Tip. Enzi hizo napiga Trip za Ujiji to Bagamoyo.
 
Utumbo wa binadamu kiunoni, aahh, mkuu hizi fix tafuta watoto wa darasa la 3😂
 
Nakumbuka sana mimi nilikuwepo wakati wa huo, nilivaa utumbo wa jamaa mmoja mnene basi nikawa kama nimevaa sketi
 
Tumetoka mbali sana .

Enzi hizo kondom ilikua utumbo wa kondoo.
 
Back
Top Bottom