Mavoko: Nitakipiga brush kimombo changu, sitaki kuumbuka kama ilivyonitokea London

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969

Kiingereza ni lugha inayotupa tabu Watanzania wengi na hakuna anayebisha kuwa kimekuwa kikitukosesha fursa nyingi za kimataifa au kujikuta tukiumbuka.
Rich Mavoko ni mmoja wao na amesema atalazimika kufuata njia ya bosi wake, Diamond ili kujinoa zaidi kuepuka kuumbuka siku za usoni.

“Mwaka jana nilienda London, nikakutana na mtu anaongea Kiingereza pale pale lakini mbona kuna vitu sivielewi anavyoongea, alikuwa ni mhindi ambaye amezaliwa kule kule. Anaweza kuuliza maswali mengi ukaelewa matatu,”
“Kizuri ambacho mimi nakijua usilete mbwembwe jibu unachokielewa kwa time aliyokuuliza, kwahiyo kuna umuhimu sana kwasababu hatuwezi kufika bila kujua hicho kitu,” ameongeza.

Rich Mavoko ana elimu ya kidato cha nne na amedai kuwa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu za kiuchumi.

Diamond naye amewahi kusimulia jinsi alivyowahi kuumbuka miaka kadhaa iliyopita wakati Kiingereza chake kilikuwa cha kuchechemea hali iliyomfanya apate hasira ya kujifunza. Leo hii hitmaker huyo anakipiga kimombo kama kawaida!
 
Kimombo ni matatizo sana jamani. Mimi nilikua mzungumzaji mzuri sana wa kimombo miaka mingi hadi mwaka jana baada ya Lowassa kupoteza urais akili yangu ikavurugika maneno yote ya kimombo yaliyokua kichwani yakatoweka.

Sasa nataka nianze moja kujifunza kimombo. Nimejifunza jambo moja kimombo hakitaki uwe na msongo wa mawazo, vinginevyo utakipoteza.
 

Asante sana mkuu umenifanya nicheke pekee angu.
 
Mbona Waziri mkuu alishasema serikali inaajiri wakalimali kila nchi na kiswahili ndiyo iwe lugha ya kuongea kimataifa? Sioni umuhimu wa mtu kupoteza mda kwenda kusoma kingereza wakati tayari nchi unayotaka kwenda utaenda kuwakuta hao wakalimali
 
Utakuta mwalimu anayekufundisha lugha ya Bi Eliza naye hajui kitu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] uwiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…