Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MAVUNDE CUP 2024
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ,Diwani wa Kata ya Ng’ongh’ona Mh. Loth H. Loth pamoja na Diwani wa Viti Maalum Mh. Janeth Kusaduka na viongozi wa CCM kata leo wameshiriki katika fainali za Mavunde Cup Ngh’ongh’ona 2024 ambapo Timu ya Itamba FC imeibuka bingwa wa mashindano kwa kuifunga Timu ya Ng’ox FC kwa changamoto ya mikwaju ya penalty 4-3.
Mh Mavunde ameonesha dhamira yake ya kuendelea kuanzisha mashindano mbalimbali katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wa Dodoma.
Akitoa maelezo ya awali Diwani Loth. H. Loth amesema mashindano hayo yamesaidia kuwaleta vijana wengi pamoj na kuchochea uibuaji wa vipaji katika kata hiyo na kuchukua fursa hiyo kumuumna Mbunge Mavunde kuendelea kufadhili michezo katika kata hiyo.