Mavunde CUP 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MAVUNDE CUP 2024

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ,Diwani wa Kata ya Ng’ongh’ona Mh. Loth H. Loth pamoja na Diwani wa Viti Maalum Mh. Janeth Kusaduka na viongozi wa CCM kata leo wameshiriki katika fainali za Mavunde Cup Ngh’ongh’ona 2024 ambapo Timu ya Itamba FC imeibuka bingwa wa mashindano kwa kuifunga Timu ya Ng’ox FC kwa changamoto ya mikwaju ya penalty 4-3.

Mh Mavunde ameonesha dhamira yake ya kuendelea kuanzisha mashindano mbalimbali katika Jiji la Dodoma kwa lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana wa Dodoma.

Akitoa maelezo ya awali Diwani Loth. H. Loth amesema mashindano hayo yamesaidia kuwaleta vijana wengi pamoj na kuchochea uibuaji wa vipaji katika kata hiyo na kuchukua fursa hiyo kumuumna Mbunge Mavunde kuendelea kufadhili michezo katika kata hiyo.

 
Haya mashindano hayawezi kusubiri Kombe la Muungano Zanzibar limalizike ili bàadhi ya timu zije kushiriki?
 
Hii ndio giving back to society pekee ambayo tunapewa na ccm imagine hivi Sasa huko nje
1.barabara za mitaa na zile kuu hazipitiki(hii ni tangu uhuru)
2.Shule hazieleweki zinafundisha kiswahili au kiingereza(hii ni mda mfupi baada ya uhuru)
3.Hospital (zahanati)kitachokupa unafuu ni kiasi cha pesa ulicho nacho nje ya hapo ni Panadol na antibiotics.
4.Utawala Bora hakuna Kila siku ni kamata funga kamata funga(tumeona na kujua Sasa kuwa baracks kumbe Kuna mochwari)
5.Rushwa hii imeota mizizi plus dhurma Kila siku raia wanadhurumiwa
6.Uhusiano wa kimataifa hata sielewi tuko poa ama ni tia maji tia maji.

kitu pekee watarudisha kwetu baada ya miaka 5 ni kombe la mbunge diwani n.k

maji hakuna kabiiiiiiisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…