Ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua madini (Shaba) Nala Mkoani Dodoma ni mkombozi wa wachimbaji wadogo na unakwenda kutibu changamoto katika eneo la kimadini
Waziri wa Madini Anthony Mavunde ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua Kiwanda hicho cha Uchenjuaji madini aina ya Shaba kilichopo Kata ya Nala nje kidogo ya jij la Dodoma kinachojengwa na kampuni ya Shengde.
"Uwepo wa kiwanda hiki ni sehemu ya mkombozi wa mchimbaji mdogo ambaye kwanzae atapata uhakika wa eneo la kupeleka malighafi na itamsaidia kumpunguzia mwendo na taratibu nyingine kwa sababu soko litakuwa karibu" - Mavunde