Mavuvuzela ya Katiba Mpya namma yanavyowachanganya wananchi

Joined
Apr 22, 2019
Posts
12
Reaction score
8
WanaJF,

Uzi nauandika nikiwa na hofu ya misleading kubwa ktk suala hili la Katiba Mpya, ni kweli Katiba Mpya ni muhimu sana kwa kuwa ya sasa ina matundu makubwa sana lakini nachosikitika kuchukuilwa kwa agenda hii kama mradi wa kisiasa kwa vyama vya upinzani na waliopoteza mvuto wa kisiasa kwa miezi hii minne ya SSH kutaka kutumia hoja hii kama mtaji wao wa kisiasa

Hoja nyingine wanabodi sisi wananchi tunakurupuka ktk agenda zetu na hii inaonesha tunapandikiziwa ajenda 2020 CCM ktk ilani yao haikuwepo suala la Katiba Mpya lakini hatukupiga kelele suala la Katiba Mpya leo hii tunamshinikiza SSH alete katiba mpya
 
Unataka kusema CCM na ikani yao wako juu ya mahitaji ya wananchi, kwamba kinachowekwa kwenye ilani ya CCM ndio final bila kujali nini wananchi wanahitaji kwa wakati husika?
 
WanaJF,

Uzi nauandika nikiwa na hofu ya misleading kubwa ktk suala hili la Katiba Mpya, ni kweli Katiba Mpya ni muhimu sana kwa kuwa ya sasa ina matundu makubwa sana lakini nachosikitika kuchukuilwa kwa agenda hii kama mradi wa kisiasa kwa vyama vya upinzani na waliopoteza mvuto wa kisiasa kwa miezi hii minne ya SSH kutaka kutumia hoja hii kama mtaji wao wa kisiasa

Hoja nyingine wanabodi sisi wananchi tunakurupuka ktk agenda zetu na hii inaonesha tunapandikiziwa ajenda 2020 CCM ktk ilani yao haikuwepo suala la Katiba Mpya lakini hatukupiga kelele suala la Katiba Mpya leo hii tunamshinikiza SSH alete katiba mpya
labda ni wewe unapandikiziwa ila sisi tuko sawa tunahitaji katiba mpya bila kujali hayo makundi ya kisiasa unayozungumzia.
 
Hiv nyie watu mna matatizo gani, huwa mnawaza kwamba hiyo katiba ikipatika ni kwa manufaa ya watu fulani au ni kwa watanzania wote na vizazi vijavyo!

Unafikiri hata ukiwa kiongozi ndani ya CCM utakaa hapo.daima?

Angalieni pia na watoto na wajukuu zenu, sio kuona kwenye pua tu!
 
Back
Top Bottom