LGE2024 Mawakala wa CHADEMA Arusha ngoma nzito, wadai kukosa fomu za kiapo

LGE2024 Mawakala wa CHADEMA Arusha ngoma nzito, wadai kukosa fomu za kiapo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Mwenyekiti wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya kaskazini Godbless Lema pamoja na wanachama wa chama hicho wamefika katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Arusha baada ya mawakala wao kuapishwa na kuto kupewa Fomu licha ya kuwa siku ya uchaguzi ni kesho.

Akizungumza wakati akiwa nje ya ofisi hizo Lema amesema kuwa hawata toka katika Ofisi hizo mpaka wapewe Fomu hizo.

PIA SOMA
- LGE2024 - Godbless Lema: Viongozi wa CHADEMA Arusha wamenyimwa Viapo vya Mawakala siku moja kabla ya Uchaguzi
 
Hahaha CCM wanajiuliza hawa watu huwa wanatoka wapi? Miaka yoote hiyo wako peke yao huwa wansema CHADEMA iliishakufa, ikifika nyakati za uchaguzi wanashangaa nyomi hilo!.

Huwa wanamdanganya SSH kuwa kesha kuwa rais, wakati wao wenyewe hawana uhakika wa nafasi zao.

Kam CHADEMA iliisha kufa basi muwe fair kwa hayo masalia ya CHADEMA ili muyashinde kwa haki, hawataki.
 
Chukua funzo hili kuelekea 2025. Jiandae vizuri. Wakati huo hakuna kucheka na mbwa yeyote.
 
Tulionya na kujiuliza tangu mwanzo kuwa ""kwann chadema inabariki dhambi ya ubakwaji wa demokrasia kwa kushiriki uchaguzi kwa katiba ya sasa na tume hii ya uchaguzi?""

Bora tukae hata miaka 20 tukiipwmbania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kuliko kushiriki chaguzi ambazo mwisho wake ni dhulma ama huruma.
 
Hao watakuwa wamskimbia na kujificha ili wasipate fomu🤔
 
Tulionya na kujiuliza tangu mwanzo kuwa ""kwann chadema inabariki dhambi ya ubakwaji wa demokrasia kwa kushiriki uchaguzi kwa katiba ya sasa na tume hii ya uchaguzi?""

Bora tukae hata miaka 20 tukiipwmbania katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kuliko kushiriki chaguzi ambazo mwisho wake ni dhulma ama huruma.
Usuburi ili uletewe kwenye sahani? Ajabu kwelikweli.
 
Back
Top Bottom