Mawakala wa Utalii wapaza sauti Taasisi ya Kilimanjaro Porters Assistance Project (KIPAP) inavyowachafua huko Ulaya

Mawakala wa Utalii wapaza sauti Taasisi ya Kilimanjaro Porters Assistance Project (KIPAP) inavyowachafua huko Ulaya

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Mawakala wa Utalii mkoani Kilimanjaro, wameitaka serikali kufanya uchunguzi na kutoa tamko rasmi juu ya uwepo wa Taasisi moja inayoendesha harakati za kuwachafua kwa mawakala wa Utalii Ulaya.

Taasisi hiyo iiitwayo, Kilimanjaro Porters Assistance Project (KIPAP) imetoa orodha ya makampuni ya wakala wa utalii nchini kwenye wavuti yake na kuwataka wageni wasipate huduma kwa makampuni ya wakala wa Utalii ambayo si mwanachama wake.

Orodha hiyo imewaibua mawakala wa Utalii na viongozi wa vyama vya wapagazi na kuhoji mamlaka iliyonayo Taasisi hiyo ya kuwaamulia wageni kampuni ya kuwahudumia.

Malengo ya KIPAP ilikuwa ni kusimamia maslahi ya wapagazi wanaobeba mizigo ya watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.

Lakini kwa Sasa KIPAP inadaiwa kuwapa angalizo wageni kutotumia makampuni ambayo hawafanyi nayo kazi .
Wamedai kuwa ,wageni wamekuwa wakipewa taarifa kuwa makampuni mengi ya hapa nchini hayana uaminifu ya yamekuwa yakipoka haki za wapagani ikiwamo kuwapa mishahara midogo.

Hata hivyo Meneja wa KIPAP, Kelvin Salla amepuuza madai hayo na kusisitiza kuwa wanaolalamika ni wale ambao wanaminya haki za wapagazi.

Akizungumzia hilo, Katibu wa Chama cha Wapagazi Tanzania (TPO), Loishiye Mollel anasema KIPAP inafanya kazi kinyume na taratibu kwani biashara ya utalii ni haki ya kila Mtanzania kufanya kwani soko la Utalii lipo wazi kwa kila mtanzania anayetimiza masharti ikiwamo kuwa na Leseni (TALA) na si vinginevyo.

"KIPAP inapofanyakazi ya kuwaamulu lazima wawe chiini yao naona ni namna gani biashara ya utalii inakwenda kuharibirika"

"Mwisho wa siku tutakuwa tunamtegemea mtu mmoja kutuletea wageni Tanzania kitu ambacho ni kinyume na taratibu kabisa "

"KIPAP haiwezi kusimama na kusema inawasaidia porters pekee yake,Ile ni project na project haina wanachama"

"Kinachofanyika pale naweza kusema kama ni dharau kwa Watanzania .

Katibu huyo ameonya kuwa hatua hiyo isipodhibitiwa inaenda kulete mdhara makubwa kwenye Utalii kwani Taasisi hiyo inaweza kujipanua na kujionia kama ndo pekee mwenye jukumu la kuleta wageni nchini.

"Mwisho wa siku akipanuka sana atakuwa yeye ndiye anasema na si watanzania wanasema lakini raslimali zote za kupanda mlima na maeneo mengine watanzania wanahaki na hakuna sababu ya kuulizwa uko KIPAP"

"KIPAP siyo sheria ya nchi ni sawa na kuuliza mtu unaleseni ,yaani KIPAP inataka Leseni ya kufanya biashara ya utalii ,hii ni hatua mbaya sana na kama inawezekana kitu hiki kisitishwe mara moja",ameonya.

Edson Matauna (Mpemba ) ni mwenyekiti wa Chama cha Wapagazi Tanzania (TPO), anasema mpaka Sasa chama chao kinao wanachama hai 16 elfu wanaolipa ada na jukumu lao ni KUHAKIKISHA maslahi yao yanalindwa ikiwamo mishahara na posho (Tip) ambazo hutolewa na wageni.

Kwa mujibu wa Mpemba TPO ni muunganiko wa vyama vya wapagazi, Kilimanjaro Mountain Porters Society na muungano huo ulikuwa ni maelekezo ya serikali kwa wapagazi kuwa na nguvu ya pamoja.
 
Back
Top Bottom