Mawakala wanaouza laini zilizokwishasajiliwa kwa alama za vidole wamesajili laini hizo kwa vitambulisho vya nani?

Gemini Are Forever

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
1,508
Reaction score
2,619
Heri ya Krismas na Mwaka mpya wanaJF!

Usajili wa laini kwa alama za vidole umekuwa changamoto kubwa sana miongoni mwetu hapa nchini. Kutokana na hilo watu wamekuwa wanachukua njia mbadala ili kuepuka kufungiwa laini zao.

1. Baadhi huwachukua marafiki/ndugu/jamaa wenye vitambulisho na kwenda kusajiliwa laini zao. (Usajili ni sh. 1000/=)

2. Kuna mawakala wanauza laini zilizokwishasajiliwa ambapo laini moja inauzwa elfu 5+ (Nilishuhudia kwenye mnada fulani wakala ameuza laini 20+ ndani ya nusu saa).

Je, hawa mawakala wamesajili hizo laini kwa vitambulisho vya nani?
 
Mimi naomba kujuzwa kama kuna uwezekano wa kujua idadi ya line zilizosajiliwa kwa namba yangu ya nida
Maana sijawahi kuweka kidole mara moja kwenye vile vimashine ikakubali yan ni kurudiarudia tu ila ninachokuwa makini kusoma line inayosajiliwa naakikisha hagusi line wala simu nyingine tofauti na yangu
Wajuzi mtujuze wanawezaje kusajili line nyingine na wewe uko hapo hapo na line niyako tu wakala hagusi simu nyingine totouti na yangu?
 
Heri ya Krismas na Mwaka mpya wanaJF!

Usajili wa laini kwa alama za vidole umekuwa changamoto kubwa sana miongoni mwetu hapa nchini. Kutokana na hilo watu wamekuwa wanachukua njia mbadala ili kuepuka kufungiwa laini zao.

1. Baadhi huwachukua marafiki/ndugu/jamaa wenye vitambulisho na kwenda kusajiliwa laini zao. (Usajili ni sh. 1000/=)

2. Kuna mawakala wanauza laini zilizokwishasajiliwa ambapo laini moja inauzwa elfu 5+ (Nilishuhudia kwenye mnada fulani wakala ameuza laini 20+ ndani ya nusu saa).

Je, hawa mawakala wamesajili hizo laini kwa vitambulisho vya nani?
Ulitoa taarifa wapi au ulishia kuangalia tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana mawakala wanaouza line zilizosajiliwa wameunganisha mipango huko NIDA au wamepata kitambulisho cha mtu hata aliyefariki basi wanaendelea kusajili maline. Ujue hiyo komputa yao inasajili tu ikiona upoNIDA haijali ni laini ngapi.NI HATARI KAMA MTU HUYO YUKO HAI UHALIFU UKIFANYIKA ATAHUSISHWA. Pia zaweza kuwa laini za mtego USALAMA maana wanajua wahalifu watazipenda sana za namna hiyo kumbe wanajininginiza kwenye mtego.
 
Na alama ya kidole watachukua kaburini??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KING 360 pengine hapo unaporudia rudia kuweka kidole chako, ndipo unasajili laini zingine kadhaa... Wanaweza kuziandaa namba za laini wanazotaka kuzisajili halafu wanaanza nazo kwanza. Hapo unapoambiwa kwmba inagoma, kumbe hapo ndpo unaposajili laini zingine. Ujanja ujanja tu mkuu.

NB: Ukiona taa nyekundu inawaka kwenye hvyo vimashine vya ku-scan fingerprint baada ya kuweka dole lako, tambua imekubali.
 
Back
Top Bottom