Kommando muuza madafu
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 3,216
- 7,254
Hili ni onyo dhidi ya TFF na bodi ya League.
Tunajua mnambembeleza Eng. Hersi akubali mechi nyingine ambayo hadi sasa mmeshindwa kutoa kauli tokana na tempo ya watu kuwa juu Kwa uhuni mliofanya.
Usiku huu viongozi wetu wametoa msimamo na ni kweli hakuna Derby ya ligi kuu tena kwa msimu huu.
Barua yenu ya hairisho ya mechi ina mapungufu mengi kikanuni na kisheria. Tumeamua kwa sasa kuyafumbia macho kwani kama mawakili na wanasheria ambao ni mashabiki wa Yanga tumekubaliana na msimamo wa viongozi wetu.
Tunajua kama nchi tuna michuano ya CHAN ambayo tunaiandaa pamoja na nchi za Kenya na Uganda. Pia tuna maandalizi ya AFCON ya 2027. Tunatambua kuwa ni kosa na tutasababisha kufungiwa kujihusisha na masuala ya Soka kama tutaenda mahakamani au kuingiza siasa. Ila sisi kama mashabiki wa Yanga wenye taaluma ya Sheria pamoja na mawakili tutaenda mahakamani kupinga aina yoyote ya uonevu ambayo itatolewa dhidi ya timu yetu.
Tunajua madhara yake kama nchi ila mkishindwa kutenda haki dhidi yetu tunaenda Mahakamani na kama nchi mjue tutafungiwa na hiyo CHAN tutaisikia Redioni.
Tunalieleza hilo sasa ikiwa ni mapema ili TFF na bodi ya ligi mjue mnavyochanga karata zenu katika hilo kuna athari itakuja katika nchi. Pia enyi TFF/bodi ya ligi mnatakiwa mjue kuwa lolote mfanyalo sasa baada ya kujichanganya wenyewe lina athari pia katika usalama na amani ya nchi yetu.
Wasalaam
Mimi Wakili Msomi..........
Member wa JF.
N.B
Moderators futeni tu huu uzi ila ndio msimamo wa mawakili na wanasheria mashabiki wa Yanga.
Tunafuatilia kila kitu kwa umakini wa hali ya juu.