Mawakili na wanasheria wanayo nafasi kubwa ya kuboresha utawala bora nchini

Mawakili na wanasheria wanayo nafasi kubwa ya kuboresha utawala bora nchini

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2023
Posts
441
Reaction score
1,065
Hawa watu wakifungua kesi nyingi nyingi zinazowahusu polisi, wakuu wa wilaya, mawaziri, wakuu wa mikoa nk zitawaweka busy na zitawapa aibu angalau wataanza kukemea uonevu unaofanywa na watu wao wa chini.

Kwa wiki hizi za karibuni nchi imepitia katika heka heka nyingi ambazo ni nyingi zinaumiza na kuacha hisia za maumivu kwa wananchi

Viongozi na wanachama wa CHADEMA wamepigwa, polisi wamesababisha vifo na majeruhi kule lamadi, watu wamesekana kutekwa na kupotezwa, watu wamebambikiwa kesi

Pamoja na matukio yote haya, ukisikiliza kauli za viongozi huoni matumaini ya kukata mzizi wa haya

Kundi pekee linaloweza kusaidia haya kupungua na hatimaye kuisha ni mawakili na wanasheria na si wanasiasa. Hawa tukiwategemea tumeisha.

Mwabukusi asingekimbilia mahakamani leo asingekuwa rais wa TLS

Hali ikibaki hivi hivi hakuna kitakacho badilika
 
Back
Top Bottom