Mawakili wengi wa ni wavivu

Mawakili wengi wa ni wavivu

Mdanganywa

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
620
Reaction score
342
Nimeiona tabi hii ya mawakili. Kesi napokaribia na wako karibu na cumba cha kuingia wakili anamchukua mteja wake na wanaanza kuongea na kupanga jinsi ya kushambulia hoja za mpinzani.

Ukipima muda utaona kwamba wametumia si zaidi ya dakika tano.

Huu ni uzembe. Uzoefu wangu unaonyesha kwamba mawakili wengi hawajiandai vya kutosha. Hivi zile dakika tano zinakusaidia nini, na unajua nini wakati kesi ina detalis nyingi.

Matokeo yake wakili anaipeleka kesi katika mtindo wa "technicality", yaani mbinu za utaratibu wa kimahakama. Na mtindo huu haujalishia kwamba wewe una haki au la. Na unaweza kweli ukashinda kesi bila kujadili hoja hata moja za kesi yako.

Mtindo huu unasababisha kesi ichukue muda mrefu, yaani badala ya miezi miwili, kesi inaenda hata miaka miwili.

Enyi mawakili, acheni uvivu wa kusoma kesi mjikite na uhalisia wa kesi yaani "substansively".

Malalamiko ya wateja yameanza kwa wanaoliona hilo na mimi sijasikia mmoja, ni wengi tu.

Usipokuwa mwangalifu basi unaweza kukuta kesi yako unashindwa kwa wakili kuendekeza "technicalities", kwa sababu hajiandai na kesi akaielewa kesi ilivyo.

Acheni tamaa ya pesa. Wakili ukimfuata ofisini unakuta ana wageni kibao na ukimbahatisha unapata dakika hazizidi 15!

Uwakili ni taaluma lakini ukizidisha biashara basi matokeo yake kesi unazipitia juujuu unaishia kuvizia "technicalities".

Eny mawakili wa Tanzania, rekebisheni tabia yenu.
 
Back
Top Bottom