KERO Mawasiliano ofisi za umma ni changamoto sijui kama Rais analijua hili?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hapo ndo nachoka kabisa. Kazi zao ni nini hawa kenge?
Mojawapo ni kuiuza taasisi.....ikiwemo hiyo kuhakikisha kila taarifa inayohitaji toka ndani ya taasisi yao inawafikia wanaohitaji
 
Nilituma email halmashauri Moja nakaribia Mwaka sasa sijajibiwa

Nimetuma msg kwenye page yao IG. Imekuwa delivered and seen ila hawajibu kitu.
 
Hata emails na msg kwenye mitandao ya jamii nazo hawajibu na zimekuwa seen kabisa.
Issue hapa ni tabia za wafanyakazi,tatizo kubwa ni ubinafsi,mtu anaangalia tumbo lake na sio maendeleo ya taasisi anayoifanyia kazi,mtu huyo huyo kama ingekua ni Kampuni yake binafsi,basi angekujibu hapo hapo,

Matatizo mengi yanasababishwa na ubinafsi,humo kwenye ubinafsi ndio unakuta mtu hajali,anaweza kula rushwa bila kuangalia taasisi inapata hasara ngapi kwa kula kwake rushwa ili afanikishe jambo kwa maslaha yake,uzembe,kutokujali..

Nafikiri haya mambo yaanze kufundishwa kuanzia watoto wadogo wakiwa Shuleni,kuwabadili wakubwa tabia ni kazi ngumu sana.
 
Sifa zote mnataka apewe Rais lawama apewe nani? In fact sijasema ni swala la rais bali nimeuliza Rais anajua madudu yanayoendelea kwenye hizi taasisi? Yeye anapambana kuvuta wawekezaji ila anakwambishwa na watu wake. Nani atawawajibisha?
Anajua sana Kwa sababu Hilo ni tatizo la kimfumo ambalo linaanzia na asili ya Mtanzania kutojitambua na kutambua wajibu wake.

Pia unaweza Kuta taasisi Hazina maafisa Habari wenye weledi.
 
Waki out-source kwa watu kama Kenya watapata mafanikio. Wabongo nuksi. Bongo unaenda hata duka la mtu binafsi anakuhudumia kama amelazimishwa!
 
Usije shangaa kukuta mleta uzi ni mwalimu ambaye haingiagi kwenye vipindi ama ni daktari ambaye hatulii kwenye kituo cha kazi,INCHI/inji hii.....
 
Nilishawahi kupiga Ofisi za NIMR Hola

Nilishawahi kupiga Ofisi za NIDA Hola

Nilijiuliza maswali mengi yalokosq majibu mpaka leo navyoona post hii

*SIJUI TATIZO NI NINI
 
Ofisi nyingi za kwenye nchi yetu ni mpaka uende physically ndiyo 'angalau' unaweza fikisha ujumbe wako,

Na hata hiyo ya wewe mwenyewe kwenda bado haiko guaranteed kuwa suala lako litapata ufumbuzi kwa haraka, ni lazima uzunguke kwanza kama chinga, uteseke weeeeh' it's like they're doing you a favor hata pahala pa kufanya majukumu yao.!!
 

I couldn't agree more, mkuu. That's the long-term solution. In the meantime, wa outsource hii service huku watoto wakifundishwa kwa vizazi vijavyo.
 
Kama ni kero ,hii ninkero 100% .

Ikulu ya chamwino,ukipiga simu haipokelewi.
 
Usije shangaa kukuta mleta uzi ni mwalimu ambaye haingiagi kwenye vipindi ama ni daktari ambaye hatulii kwenye kituo cha kazi,INCHI/inji hii.....

The pot calling the kettle black.
 
Nilishawahi kupiga Ofisi za NIMR Hola

Nilishawahi kupiga Ofisi za NIDA Hola

Nilijiuliza maswali mengi yalokosq majibu mpaka leo navyoona post hii

*SIJUI TATIZO NI NINI

Unatumia muda na vocha zako na bado hawapatikani au hawajibu. Nje namba za taasisi kama hizi ni Toll free yani hata ukipiga kwa simu yako hukatwi vocha wanapokea na kukupa majibu. Huku Tanganyika wanaona kupokea tu ni kazi au kulipa bill ya simu na hili ni shirika la umma. Smh
 

Changamoto.
 
January Makamba na Maharage Chande watuambie walichofanya Tanesco, So far Tanesco wanajitahidi kwa 80%

Kwingine kote takataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…