Pole, unataka mawasiliano ya ofisi gani?Zipi hizo?
Nsaidieni mawasiliano wakuu anaumwa anataka apae akajitibie kwanza
Wale hawapokei simu.Habari zenu wakuu?
Kwa heshima na taadhima ninaomba mnisaidie namna ninaweza kuwasiliana na makao makuu ya Mfuko wa Mafao ya Kistaafu wa Umma -PSPF (sijui nitakuwa sahihi kwa kifupi chake).
Nimejaribu kuangalia contacts zao online sijapata cha kueleweka zaidi ya ofisi za mikoa tu.
Kuna mzee wangu amekwama kupata mafao yake kwa mda mrefu tangu astaafu ameomba nimsaidie ili ajaribu kufwatilia nini kinamkwamisha maana ni mda mrefu sasa ofisi ya mkoa inampatia majibu yasiyoeleweka.
Nchi ya hovyo hiiMara anayehusika na calculations ndo tatizo...file linakaa meazani kwa mtu mmoja miezi 4 kwelii??? Hata pension tu ya mwezi hajapata tangia
Hii serikali naweza andika vibaya nkatafutwa na wasioonekana
kati ya watu wajinga, wewe umo.Tunyweni bia
Umenena vyema. Mwaka wa saba huu bado Baba yangu anahangaika kufuatilia mapunjo ya pensheni ya mwezi na malipo ya mkupuo. Majibu anayopewa ni kwamba anayehusika na calculations bado hajalifanyia kazi faili lake. Yaani karne hii ya 21 pamoja na kompyuta kibao ofisini hapo wanashindwa kukokotoa hesabu nyepesi kiasi hicho. Baba anayo kompyuta mpakato yake aliyoinunua mwaka 1999 (karne ya 20) ambayo ina kile kikokotoo cha iliyokuwa PPF. Akiingiza namba zinazohitajika jibu linatoka ndani ya nusu sekunde. Iweje hawa wenye kompyuta za kisasa kabisa washindwe kupata jibu hilo kwa kipindi cha miaka sita!! Kiukweli ninyi PSSSSSF, Mungu anawaona mnavyowatesa wazee wetu.Mara anayehusika na calculations ndo tatizo...file linakaa meazani kwa mtu mmoja miezi 4 kwelii??? Hata pension tu ya mwezi hajapata tangia
Hii serikali naweza andika vibaya nkatafutwa na wasioonekana