Natumaini wote mmekua na jumapili njema!
Nwy kwa ndugu/jamaa/marafiki na mwenzi wako nini unachukia sana linapokuja swala la mawasiliano (simu au hata email) ?!
Binafsi sipendi
1) unapompigia mtu alafu asipokee kwa sababu yoyote ile alafu hata baadae ashindwe kukupigia au hata kukutext for no reason at all (hamna matatizo ya charge wala credit) mpaka umtafute tena mwenyewe.
2)Unapompigia mtu anakwambia yuko bize atakutafuta akimaliza mambo yake alafu hafanyi hivyo.
3)Mtu anaejibu text/email ndefu ya maana kwa neno moja...Owkey..Poa..Sure and the likes !Mara moja moja mi hua nadondoka hapa!
4)Mtu asiyepokea simu hata kutwa bila kukupa sababu ya kuacha kupiga...pokea sema huwezi/hutaki kuongea.Hapa kama sio kawaida mtu anaweza patwa na wasiwasi!
5)Mtu anaekasirika ukimwambia kuna simu nyingine unahitaji kupokea/piga mara moja!6)Mtu anaebeep bila sababu ya msingi.
7)Mtu anaeforwad email/text ndeeefu zisizo na maana.
8)Mtu anaeomba kutumia simu yako alafu anaanza kuangalia salio au kuchungulia msg zako(huyu sio mpenzi)...rafiki tu au ndugu.
9)Mtu aaetoa namba yangu ya simu kwa mtu anaeiulizia bila kuniuliza mimi kwanza.
10)Mtu asiejua kujibu msg za watu wengine ila yake ukiipotezea tabu.
Chache zinazonihusu naanza kujirekebisha!!
So wewe zipi sinakuhusu na zipi hupendi..........?!
Umesema mambo ambayo yanakera kwa kweli.
Lakin nadhani kuna vitu ambavyo vinasababisha yote hayo.
1) Ana shughuli nyingi/Kazi nyingi ambazo zinamfanya asahau kutekeleza aliyoahidi
Hii ni sababu ambayo hata mimi inanitokeaga tena mara nyingi tu. Umepiga simu nipo ktk seminar, tena mbaya zaidi mi ndio facilitator si rahisi kukujibu hata nukta. Kuna sababu zingine kama misiba, ajali n.k.
Na mbaya zaidi itokee waliopiga wakati huo ni wengi zaidi (tuseme 25).
Kama ni simu utatakiwa upigie wote 15, au kama ni text basi u-text 15 times!!!! Si rahisi kuridhisha kila mtu.
Na hata kama simu ilipokelewa na kuahidiwa maongezi zaidi baadae, mara nyingine si rahisi. Uchovu wa kazi na majukumu utakufanya utake kupumzika badala ya kutafuta watu ulioahidi kuwapigia.
Kama upo ktk majukumu yako, huwezi kujibu msg ndefu kama inavyotakiwa. Majadiliano marefu mara nyingi yapaswa muongee ana kwa ana, kama ikitokea kwenye mitandao itashindikana kutokana na majukumu mbalimbali.
Lakin msisitizo ni kuepuka kumpigia simu mtu ambaye hujawahi hata kumbeep miaka nenda rudi halafu first call unamwambia unashida, unaomba akusaidie pesa yake. Mfano michango ya harusi, kipaimara n.k. Hata mi nakupotezea hata kama nilikuahidi kukuchangia.
2) Hana muda wa kuongea/kuchat na wewe muda mrefu (Umuhimu wako kwake ni mdogo)
Ukiondoa sababu ya kwanza hapo juu, sababu nyingine ambayo ni more likey ni hii.
Si rahisi hata kidogo kuambiwa maneno haya, lakin yapaswa usome alama za nyakati.
Si rahisi kumwambia mwenzako " . . ebwana eeh, sina muda na wewe saa hiz"
Au " . . . sitaki simu zako bwana, unanisumbua"
Badala yake jifunze kusoma tabia yake. Ukiona kila siku unakaushiwa namna hiyo ujue umeambiwa MIND YO BIZNES
Unapiga simu wiki nzima kapokea mara 1 tu, ume-text msg 200 umejibiwa 3 tu . . . unataka ishara gani tena za kuelewa kwamba umeambiwa "STOP FOLLOWING ME"??
3) Others . . . .
Mtu anaekasirika ukimwambia unapiga/unapokea simu nyingine:
Binadamu tumweumbwa na wivu, tamaa na sometimes kutaka kupewa attention zaidi.
Tumeongea dk 4 ktk simu, na mara katikati ya maongezi unaniambia " Kata simu kuna mtu muhimu sana ananipigia" au unakata mwenyewe bila taaarifa yoyote, halafu baadae unaniambia "Nilikuwa naongea na mtu fulani hivi (huweki wazi)" unategemea hapa nitajisikiaje??
Kama kuna simu unataka kupiga/kupokea basi weka wazi kwamba "Mama ananipigia mara moja, ngoja nimsikilize anasemaje, tutaongea nikimalizana nae" Au "Napigiwa simu kutoka ofisin, ngoja nipokee mara moja" Au "Mpenzi wangu ananipigia".
Weka mambo wazi uondoe uwezekano wa kueleweka vibaya.
Lakin kama bado ukisema hivyo haelewei basi ANA JAMBO SI BURE
Ku-beep kuna sababu nyingi pia.
- Labda kakosea jina la kupiga, akalazimika kukata mara anapogundua kakosea (majina kufanana). Hii itaonekana kama beep kwa mpigiwa
- Ana tatizo la vocha anaomba umpunguzie. Hii labda mhusika hauji kutuma TAFADHALI NIPUNGUZIE
- Amekumiss sana ila hana vocha ya kuku-text wala kuku-call (yaani anakusalimia)
- Anakufahamisha ana tatizo, hana vocha ya kupiga wala ku-text hivyo anasisitiza UMPIGIE MAPEMA (anakubip mfululizo)
- Ndo anaanza kushika mobile phone mara ya kwanza
Ukiondoa sababu ya kwanza na ya nne, hizo nyingine zina picha ya usumbufu zaidi.
Ku-fowardiana msg:
Hii kikawaida ina lengo la kuchekeshana (msg za ucheshi) au kuelimishana (msg za maneno ya hekima, busara au maneno ya kiimani)
Msg zingine za ucheshi haziwachekeshi wahusika badala yake zinawakasirisha.
Mfano unamtumia mtu msg inasema
" Em Bii Ooo alikuwa anabishana na kiatu. Kiatu akasema "Mimi nateswa balaa, nasuguliwa na kukanyagwa hadi chooni na vinyesi". Lakin Em Bii Ooo ana mjibu " mimi ndio balaa zaidi, kwanza nafungiwa kwenye chumba bila hewa wala mwanga, nikitolewa hapo naingizwa chumba kingine cha giza, hakina umeme, humo nasuguliwa weeeeee . . . .mpaka natapika, halafu narudishwa chumba cha awali. Sinyweshwi hata maji ya kunywa wala kulishwa"
Wengine watakasirika, wengine watacheka.
So let them know kwamba hupendi hiki na kile, wasipoelewa chukua hatua kubwa zaidi
Kuchungulia msg/ Salio:
Hili lina sura ya kuchunguzana maisha au sura ya kiumbea zaidi. Sijui lengo ni nini hasa lakin linaonyesha nia ya kutaka kukutangaza kwa wengine jinsi ulivyo au unavyoishi. Mtu anaangalia salio na msg anakuta balance ni Tsh 25,500/= line ya tigo, ya Voda anakuta kuna Tsh 16,800/= na kama haitoshi anakuta msg zimeandikwa nimetuma pesa Tsh 350,000/= kwa mtu.
Huko nje utaanza kusikia "CPU anachunwa balaa, anatuma laki 3 na nusu kila mwezi kwa demu wake". Au utaona anaanza kukupigia misele "Ooh sipiyuu niazime laki 2 ntarudisha wiki ijayo" ukimwambia sina utasikia "mbona unawatumia watu mpaka lak 7 kila mwezi, acha kunibania bana"
SAMAHANI KWA MAELEZO MAREFU