Mawasiliano.....!

kwakweli kiongozi, hata kama ni janga la kitaifa,
lakini inakera mpaka inapitiliza,

Halafu mbaya zaidi anakupigia akikwambia,
''nimekuta missed calls zako, kwani ulikuwa unasemaje''?

hapo ujue labda ni baada ya masaa kama mawili hivi!!!!!!

Hao ndio wake zetu bana! yaani mtu unaweza kuwa unakabwa njiani jamaa amedai mshiko, umejikaza unampigia waifu simu ili alete mshiko eneo la tukio, kumbe waifu simu kaweka kwenye handbag na yeye yuko kwenye kioo anaweka make up. siku ya pili anajifanya kukulilia msibani hehehe hii tabia hata Lizzy apinge wanayo wanawake wote.
 
Khaaaaa!
Ndo tunaita kutongoza kusikotongozeka
:biggrin1:
heheeh CPU bana! yaani akili iko kwenye kutongoza tu! hapa tunaongelea maslahi ya taifa kupitia mitandao ya simu bana.

offu topik: kuna rumours kwamba nataka kupewa umod, mnaombwa kunipigia debe la nguvu.
 
Reactions: CPU
heheeh CPU bana! yaani akili iko kwenye kutongoza tu! hapa tunaongelea maslahi ya taifa kupitia mitandao ya simu bana.

offu topik: kuna rumours kwamba nataka kupewa umod, mnaombwa kunipigia debe la nguvu.

Taifa lolote lililopiga hatua lina hesabu nzuri za kutongozana.
Tafuta data za mitongozano za UK, France (hawa jamaa ndo nouma), US na Italy
UK wameanza kuvuma juzi tu kupitia kwa John Terry, Ashley Cole na wenzake

Ili taifa liendelee lazima wadada na wakaka mtongozane kwa wingi

Offu topiki:
Utaangukia pia kama Six.
U-Mod safari hii ni kwa ajiri ya akina dada tu
 

  • Namba moja, ni private number Callers, ...nimeamua kutopokea ujinga huo.
  • Kisha, unampigia mshkaji halafu 'Icely Cold' anajibu kwa mkato i.e "safi!,""poa,""sawa,!" ...Crap!...kama 'ulikuwa' hutaki kuongea usingepokea. kalagabaho!
 

Duh Lizzy aksante sana kwa mada hii........Umenigusa sana mimi ni mbovu sana wa mawasiliano yaani sometimes najiuliza hii simu nilimiliki ya kazi gani ah!! Sometimes naisahau nyumbani nikienda kazini... na hata nikikuta misd calls labda nirespond hapo hapo ninapozikuta otherwise zikishatoka kwenye screen sikumbukagi tena..................

Ngoja nijirekebishe.
 
Ha ha ha wale wasiopokea private number (ukipiga toka nje ya TZ huandika hivyo) au namba ambayo haijui wananiudhi (Lizzy kaniwahi kuanzisha thread ningekuanzishia) unajijua naye kuzungumzia hapa
 
Hili la kupunguziana salio lisingekuwepo ingekua poa sana...zile msg hua zinaboa sana!
Alafu watu wengine ukishawapunguzia wanakubeep upige wakwambie ASANTE!!

Ha ha ha... Yaani...!
 
- Mtu mwenye line 4 za simu yani zantel, voda, tigo mara zantel ni yeye tu...sielewi jinsi mtu unawezaje kuwa na line zote hata line 3 tu!..

Wenyewe hua wanadai ni ili waweze kuwasiliana na watu wenye mitandao tofauti kirahisi....bei i suppose!

Lizzy... hiyo namba 2 nakumbuka sana kuna mtu alinifanyia i was in Nairobi muda sasa umepita;

I felt disrespected... coz nilikua namheshimu sana before!!:eek2::eek2:

I hate that....hua inaboa sana!!Bora mtu aseme tu nipo bize bila kuahidi chochote hata asipopiga unaweza kuchukulia poa tu kuliko kuahidi kitu alafu asifanye.


Hahahhaha...
HELLO....
hELLO...
We nani??
We sindo umenipigia??
Ndiooo ila we naniiii???

KAAZI KWELI KWELI!!
Mhh nat really...mi ni mzuri kujibu msg za watu isipokua kama ameniboa ndo natoa majibu ya Owkey..Fresh..Poa..Mzima..Fine.

Namba ya ndani staki nataka ya mkononi ili niwe nakuomba salio!!



Hahahaha...Kloro ana siku nzuri!!!
Unajua tatizo ni kwamba sijui wengi au baadhi ndo hua wanajisahau...mi siwezi kuiacha mbali na mimi unless sijisikii kuongea na simu na kuzima sitaki!
 

Ha ha ha...Umenikumbusha mama yangu.... Kila siku ilikuwa ni ugomvi na baba.... Kama unashida nae mchana imekula kwako...always simu iko kwa handbag...
 
  • Namba moja, ni private number Callers, ...nimeamua kutopokea ujinga huo.
  • Kisha, unampigia mshkaji halafu 'Icely Cold' anajibu kwa mkato i.e "safi!,""poa,""sawa,!" ...Crap!...kama 'ulikuwa' hutaki kuongea usingepokea. kalagabaho!

Namba mbili naichukia sana...utadhani umepiga kukopa bwana!!!

Inabidi ubadilike mamito!

Ha ha ha wale wasiopokea private number (ukipiga toka nje ya TZ huandika hivyo) au namba ambayo haijui wananiudhi (Lizzy kaniwahi kuanzisha thread ningekuanzishia) unajijua naye kuzungumzia hapa

Hahahahah...mi mwenyewe hua sipendi kupokea uknown calls ila naweka yangu isionyeshe!!
Hehehehe...hopefully ujumbe umemfikia mhusika!
 
Kweli sister Lizzy wendo great thinker nakukubali na huwa nazipenda sana post zako.
kwa hilo la mawasiliano umeagusa wengi na mimi ni miongoni mwano lkn kuanzia leo naanza kubadilika, thanks a lot!
 


Bahati nzuri sina hata moja ya tabia hizo hapo juu. Na wale wanaopenda kuforward emails zisizo za maana huwaambia mimi sipendi kabisa kuzipata emails kama hizo hivyo naomba wasinitumie tena (utakuta ni rafiki wa miaka mingi labda hamjawasiliana kwa kipindi halafu anaforward hiyo kitu hamna hata kusalimiana/kujuana habari wala nini tena nyingine zina mapicha ambayo huwezi kuangalia mara mbili!) na wamenisikia maana sijapata emails kama hizo kwa siku nyingi sana. Nachukia sana pale mtu anapotoa namba yangu ya simu au email address bila ruhusa yangu.
 
Code:
9)Mtu aaetoa namba yangu ya simu kwa mtu anaeiulizia bila kuniuliza mimi kwanza.

Hii kwangu ni kero sana.................
 

Tunamba fulani hapo juu mi pia nahusika ! natafuta njia ya kujirekibisha
 
Hizo zote tisa, KUMI kuna mdada mmoja ambaye atakuomba aangalie handset yako, then huna hili wala lile anatumia simu yako kujibeep, anaipata namba yako..kinachobaki ni usumbufu.."We nanihiino, UKO WAPI saa hizi...nina hamu na Castle-Light leo"...my hairs!!
 
Mhhh nahisi wanaume ndio zao hizi
 

ok ok ok
 
i hate Voice mails, sizitaki kabisa!

Hi, you have reached Nyani Ngabu. I am sorry I am not available to answer your call right now, but if you leave me your name, number, and a brief message I will get back to you as soon as possible. Thank you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…