Mawaziri Dkt. Pindi Chana, George Simbachawene na Ummy Mwalimu kujadili ongezeko la vifo na talaka nchini

Mawaziri Dkt. Pindi Chana, George Simbachawene na Ummy Mwalimu kujadili ongezeko la vifo na talaka nchini

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa Katiba na Sheria Dr Pindi Chana atakutana na Waziri wa Utumishi George Simbachawene na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kutafuta Suluhisho la Ongezeko kubwa la Vifo na Talaka nchini

My take: Sijajua Kwanini hawajamshirikisha Dorothy Gwajima

========


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Balozi Dk. Pindi Chana amesema amepanga kukutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kutafuta suluhisho la ongezeko la vifo na wimbi la talaka katika jamii.

Kwa mujibu wa taarifa ya takwimu ya matukio muhimu ya binadamu ya Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), takwimu inaonesha kumekuwa na ongezeko la vifo kwa wanaume vinavyosababishwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza jambo ambalo linasababisha ongezeko la watoto waishio kwenye mazingira yasiyo bora kutokana na kukosa malezi ya pande zote mbili.

Aidha, Waziri Chana amesema kwa upande wa hali ya ndoa, takwimu inaonesha ongezeko la usajili wa talaka limekuwa kubwa kwa kila mwaka jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa ukatili kwa watoto kwa kukosa malezi ya wazazi wawili.

Akizindua taarifa ya takwimu ya matukio muhimu ya binadamu pamoja na kufungua mafunzo ya uendelevu wa usajili wa watoto ya RITA mkoani Dodoma jana, Waziri Chana amesema katika takwimu za sensa kuhusu hali ya ndoa kwa mwaka huu RITA wamesajili talaka 800 ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambayo ilikuwa ni chini ya hapo hivyo ni wajibu wa Serikali kukaa na kuona wananusuru hali hii.

“Nahitaji kikao na Waziri wa Mambo ya Ndani ili tukae tuzungumze, takwimu za ajali, vifo kama tulivyoambiwa na taarifa ya RITA, tunafanyaje, haraka sana nahitaji kikao na waziri mwenzangu dadaangu Ummy Mwalimu, lazima tushee hizi data ili tupate kujua tunafanyaje.” amesema Waziri Chana.

Pia alisema kama ikiwezekana zinapopatikana takwimu za talaka wakati mwingine ni vema zipatikane na sababu ya talaka hizo ili kuona wanazitafutia vipi suluhisho.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Back
Top Bottom