BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Date::10/10/2008
Mawaziri wapishana mgodini kutatua matatizo Kahama
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi
WAKATI Waziri wa Nishati na Madini, Wiliam Ngeleja akiondoka jana wilayani hapa kumaliza mgogoro wa mgodi wa Bulyanhulu na wanakijiji wa Kakola, naibu wake ameingia Kahama kumaliza mgogoro wa wananchi wa Buzwagi na kampuni ya Barrick.
Naibu huyo, Adamu Malima ameingia jana ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali ililolitoa mwezi Mei mwaka huu la kutaka mikataba yote ya fidia kwa wananchi wa Buzwagi ipitiwe upya ndani ya miezi mitatu, muda ambao umeshapita.
Wakati naibu waziri huyo akiingia Kahama, tayari bosi wake ameondoka jana katika mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa pia na kampuni hiyo ya Barrick baada ya kushughulikia mgogoro wa wananchi wa kijiji cha Kakola wa kufungiwa umeme kama makubaliano baina ya wananchi na serikali yanavyoeleza.
Katika makubaliano hayo, kampuni hiyo ilikubali kuwapa wananchi hao huduma za kijamii baada ya serikali kukitangaza kijiji hicho kuwa ni halali kuliko ilivyokuwa hapo nyuma wakati ilipotaka kukihamisha ili kupisha mgodi huo.
Akiwa katika kijiji cha Kakola, Waziri Ngeleja alizindua mradi wa umeme ambao umegharimu kiasi cha dola 500,000 za Marekani (sawa na zaidi ya Sh500 milioni za Tanzania) zilizotolewa na Kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa BGML.
Katika uzinduzi huo, Ngeleja aliwataka Wanakijiji wawe watulivu na kujenga urafiki kati yao na Mgodi hali itakayo wajengea mahusiano mazuri ya kupatiwa huduma mbalimbali za kijamii kuliko kujenga uhasama na wawekezaji, akisema migogoro huchukua muda mrefu kuitatua.
Kabla ya kauli ya waziri huyo, meneja mkuu wa Barrick Tanzania, Deo Mwanyika aliwambia wananchi hao kuwa kampuni yake itaendelea kutoa misaada ya kijamii iwapo wananchi watajenga mahusiano ya kirafiki na mgodi huo.
Mapema mwaka jana, wananchi hao waliziba barabara zinazoingia mgodini na kuzuia magari wakidai kupatiwa huduma za kijamii ikiwemo maji , umeme, barabara. Tayari mgodi huo umeanza kutekeleza masuala hayo.
Akiwa Kahama, Naibu Waziri Malima anatarajiwa kumaliza mgogoro wa Buzwagi ambao unaendelea kuwa na mgogoro na wawekezaji baada ya wananchi kukata uzio na kuingia kwa nguvu ndani ya Mgodi huo wakitaka kulipwa fidia kw amadai kuwa walipunjwa katika malipo ya awali.
Hali ya wananchi hao kuingia kwa nguvu kwenda kuishi katika makazi yaliomo ndani ya mgodi kulimfanya kaimu mkuu wa wilaya ya Kahama, Magesa Mlongo kuwatawanya kwa nguvu wananchi hao, akitumia polisi ambao wakati fulani walifyatua mabomu ya machozi.
Baada ya Vurugu hizo, serikali iliingilia kati na kuagiza mikataban yote ya malipo ya fidia kurudiwa upya kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu.