Mawaziri waweke platform za kupokea Ushauri

Mawaziri waweke platform za kupokea Ushauri

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia,
Nashauri Mawaziri wote waweke Ukurasa (platform) hata kwenye website za wizara zao zenye sehemu mbili
1. Kupokea maoni
2. Kupokea malalamiko

Na waziri mwenyewe au msadizi wake awe anapitia mwenyewe mara kwa mara ili apate ujumbe BILA filter
Ukifuatilia huku mtaani wapo watu wenye maoni mazuri sana ya kusaidia Nchi lakini hakuna mawasiliano ya moja kwa moja; Unaweza ona wananchi wanateseka kwa kitu cha kutolea tu maelekezo kwa watendaji wa chini bila gharama yoyote.

Au pengine kuna changamoto ndogo ambazo hata kwa bajeti ya Wilaya inaweza kutekelezeka lakini ndio hivyo tena hakuna mawasiliano ni hadi Muheshimiwa Rais apite watu wasimame barabarani.

NAAMINI MAWASILIANO NDIYO KILA KITU
Labla niweke Nyongeza kuwa; namba Za simu za taasisis za Umma zilizo kwenye mtandao nafikiri zaidi ya 70% hazipatikani kwa sababu mbalimbali either ni mbovu au zilisha badilishwa; Ukituma email inabidi uende kwenye maombi ili ujibiwe.......

Hii inaonesha kuwa mawasiliano na taasisi za umma hayapo au ni madogo sana....

Wahusika wanaweza wasijue hili tatizo kwa kuwa wao humpigia muhusika direct kwa namba binafsi
 
Ni kwasababu tunamfumo wa serikali isiyo ya wanainchi inayodeal na maoni ya wachache wanaonufaika na mfumo.

MUDA UNAKWENDA, TUCHUKUE HATUA HARAKA SANA.
 
Hayo maoni yatakua hayahusu wizara ya nishati na wizara ya maji maana hakuna kero kabisa mitaani

Nasema wali wakushiba unaonekana kwenye sahani.......alisikika bwana maji akijinasibu mbele ya mkuu wake
 
Kulikuwa na toviti ya mwananchi huko nyuma, ilianzishwa enzi za Vasco Da Gama awamu ya nne, lengo lilikuwa hilo ulilobaini. Pamoja na kuingia gharama za kuianzisha na watu kuichangamkia kwa kutoa maoni, sikuwahi kusikia mtu aliyejibiwa nikiwemo mimi mwenyewe.

Ilikuja kufa kifo cha mende hata kabla ya kuanza.

Wazo na ushauri wako ni mzuri, Ila sioni ni nani au Serekali gani hiyo itakubali kuwa tayari kukosolewa. Sana mpango huo utawezesha wapigaji kuchota pesa za walipakodi kwa manufaa yao binafsi.
 
Back
Top Bottom