Jumatano ya tarehe 28 Oktoba Watanzania tuna nafasi ambayo binafsi naamini kwa wengi wetu wa kizazi hiku hatutapata tena. Ni nafasi ya mara moja katika maisha ya wengi wetu ya kufanya maamuzi sio tu ya kuchagua uongozi kwa kipindi cha miaka mitano, bali kufanya maamuzi yenye uwezekano wa kubadili historia ya nchi yetu milele.
Kwa nchi ambayo kidemografia vijana ni wengi zaidi, kesho kutwa inawapa nafasi ya kuamua sio tu miaka 5 ijayo ya maisha yao, lakini mwelekeo wa maisha yao na ya watoto kwa miaka na miaka ijayo. Mwelekeo tutakaouchukua Jumatano, bila kujali upande tutakaouchagua, kwa ngazi zote, hasa za urais na wawakilishi, utaibadilisha nchi yetu kwa vizazi na vizazi.
Sidhani kama tumewahi kuwa na uchaguzi wenye maana (consequential), unaoamua mwelekeo wa Tanzania, utanzania kwa vizazi na vizazi zaidi ya huu.
Miaka 60 baada ya uhuru, kama jamii tumefanya mengi, mazuri na mabaya, na tumefika hapa tulipofika. Pamoja na hayo, si uchaguzi wa kutazama tulipotoka zaidi ya tunapotaka kwenda.
Si uchaguzi wa kujitazama wenyewe tu, lakini mwenendo wa nchi za jirani, na za mbali, kwa walipotoka miaka 60 iliyopita, na walipo sasa. Jirani kama Zimbabwe na Uganda na kwa mawazo yangu, tuna tishio halisi (real threat) tukafanya maamuzi yatakayopelekea tuwe kama wao. Za mbali kama Malaysia (ambao walipata uhuru 1957, miaka 4 kabla yetu) Singapore (1959), Kuwait (1961), Botswana (1966), Qatar/Bahrain na UAE (1971) na leo wapo walipo, na sisi tupo tulipo.
Kutazama nje kwa kuangalia nafasi yetu kwenye mahusiano na wenzetu kimataifa yalipo, na tunapotaka yawe kesho kwa kuzingatia kwamba tuna historia ya kuwa taifa ambalo pamoja na uchanga wake, tumewahi kuwa na ushawishi kwa wengine. Kuamua kama tunawatazama wenzetu walioshirikiana na sisi tangu uhuru kama wadau wa kweli wa maendeleo na kutoka kwenye kuendelea kukumbatia itikadi za jana za kupigania uhuru na siasa za vita baridi na badala yake kudai kutoka kwao ushirikiano bora zaidi usio na hila.
Siamini uchaguzi huu ni uchaguzi wa miundombinu na huduma za jamii kama ambavyo chaguzi zilizopita zilikuwa. Ukinunua shamba, haichukui muda utaita majirani mkaazimia kupisha njia. Mtakapokuwa na uwezo zaidi, hizi njia zitakuwa za lami na zaidi. Muda utapita mtachimba visima na kuwekeza kwenye vituo vya afya. Ni hulka ya mwanadamu.
Siamini uchaguzi huu ni wa vita vya ufisadi kama ambavyo chaguzi hasa za hivi karibuni (miaka 10 au zaidi kidogo iliyopita) zilikuwa. Sijaona sababu ya kuamini kama watanzania, kwa wingi na dhamira ya kuridhisha, wanauchukia ufisadi kwa umuhimu unaufanya kuwa suala (issue) kwenye uchaguzi huu.
Siamini huu ni wakati wa kuamua kwa kufuata uchama kwa sababu matokeo ya maamuzi tutakayofanya yana uwezekano mkubwa wa kudumu (outlive) hata baada ya vyama tunavyojitanabaisha navyo kuwepo.
Naamini uchaguzi huu una maana ya msingi zaidi kuliko tulivyozoea (deeper, more substantive).
Naamini, hatujawahi kuwa na uchaguzi ambapo utambulisho wetu kama jamii, kama taifa, utambulisho wa ustaarabu wetu, utu wetu umejaribiwa (tested) kama ambavyo uchaguzi wa kesho kutwa unavyo tuhitaji (call into question).
Naamini uchaguzi huu ni mapambano ya uhuru ya kizazi cha vijana wa leo wa Tanzania (freedom fight of today's youth).
Binafsi, siwezi kwa dhamira ya dhati kupiga kura bila kufikiria familia ya Akwilina. Naamini kwa mauaji (senseless killing) ya binti yao, tumeua ndoto alizokuwa nazo binafsi na walizokuwa nazo kwake, na kama jamii, hatujawahi kuwapa haki wanayostahili baada ya jambo hili baya kutokea. Uhai ukipotea haurudi, lakini hatujawahi kuwalipa (restitution) kwa udhalimu (injustice) waliofanyiwa. Naamini hata kuonyesha dhamira ya dhati hili lisijirudie tena kwa mwingine ingewapa faraja kidogo.
Siwezi kuacha kumfikiria binti mdogo wa Ben Saanane atakayekua asijue kilichomtokea baba yake pengine kwa maisha yake yote. Kama binadamu, dhamira yangu hainiruhusu nikubaliane na familia ya Ben kukosa majibu nini kilimtokea ndugu yao (closure). Uamuzi nitakaofanya Jumatano ni kuamua kusema hapana, hata kama sina majibu kwa familia hii, nisingependa kuwa sehemu ya waliopitia na kuendelea kupitia kuwatokea wengine.
Nitaitumia kura yangu kwa dhamira nyeupe kabisa kumwonyesha mjane wa Azory Gwanda na wanae kwamba sina msaada kwao zaidi ya kumwonyesha kwamba kwenye shimo la kiza waliopo, kuna sauti inawapigania wao na kusema imetosha.
Siwezi kuacha kumfikiria Marehemu mama wa Eric Kabendera. Maendeleo ninayoyataka hayastahili kugharimu tulichomfanyia yeye na familia hii.
Siwezi kuacha kuwafikiria wengine wengi ambao wamepoteza maisha au kuumizwa bila majibu ya kiuchunguzi yanayoridhisha kutoka kwa vyombo vyetu
vya usalama. Kama yaliyotokea miaka 5 iliyopita ni matendo ya kawaida ya jinai, napigia kura jeshi la polisi lililo bora zaidi kupambana nayo badala ya kuishia kuomba wananchi watoe taarifa kama wanazo au uhalifu unatokea hata New York.
Siwezi kuacha kuwafikiria Theo Gyan na Tito Magoti, kwa ujana wao ambao kama nchi tunashiriki kuwanyanganya kila siku wanayoimaliza wakiwa ndani kwa kuwa na mawazo huru, kuwa na ndoto zisizowapendeza baadhi yetu.
Hakuna daraja au reli ya muhimu kwangu kuliko haya.
Kura yangu jumatano ni kuwatia moyo mlio kwenye mifumo yetu ya mbali mbali ya kiutawala na msiofurahishwa na mwelekeo tunaochukua kama nchi lakini nafasi mlizonazo zimewafunga mikono. Hamko peke yenu, msiache kupambana mnapoweza, kwa sababu mtakapochoka, Tanzania tunayoijua itabaki historia.
Vyombo vya upatikanaji haki na usimamizi wa sheria, nitapiga kura kuchagua Tanzania ya haki ya kweli kwa wote, na tamanio uhuru wa kweli wa mfumo wa haki, vyombo vya dola vinavyoweka maslahi wa raia kabla ya kitu chochote, kuonyesha mshikamano wangu na wale baina yenu mnaoamini kwenye haya matamanio.
Vyombo vya habari, ni rahisi kuwalaumu, ni dhahiri lawama mmezipokea za kutosha. Nitapiga kura ya kuonyesha imani yangu ya ndani kabisa ya umuhimu wa uhuru wa kazi zenu, mshikamano wangu kwenu. Kwenda kinyume na dhamira yangu hii ni kukubali chombo cha habari kuvamiwa kwa mitutu na kiongozi wa serikali dunia nzima ikitazama bila hatua kuchukuliwa kwa mhusika. Kukubali kwamba hii ni kawaida tunayohitaji kuizoea kwenye Tanzania ya kesho.
Binafsi, natarajia kupiga kura Jumatano, nikiwa na picha ya Bunge lililomaliza muda wake. Nina imani ya dhati kabisa kwenye dhana ya mgawanyo wa madaraka kama ambavyo ilidhamiriwa na katiba yetu na nyingine nyingi duniani. Siamini bunge lililopita kwa ujumla wake liliniwakilisha. Sheria zilipitishwa ambazo binafsi sina maslahi nazo kama mtanzania.
Hata pale zilipopigiwa kelele na wananchi, haikusaidia hadi pale washirika wa maendeleo walipoweka mguu chini na kupelekea zibadilishwe ndani ya muda mfupi. Sitaki Tanzania ambayo Benki ya Dunia ana sauti zaidi yangu. Sikuona jukumu la uangalizi (oversight). Dhana ya checks and balances iliwekwa kando, na badala yake, bunge kwa ujumla wake mara kadhaa lilijipa jukumu la kupiga muhuri matakwa mengi ya serikali. Kama gharama ya uamuzi wangu ni kutoletewa maendeleo, niko tayari kulipa ili angalau kuwe na uwajibikaji utokanao na uwepo wa jicho na sauti mbadala kwenye bunge lijalo.
Nitapigia kura elimu bora kwa watoto wetu inayoenda mbali zaidi ya kuhesabu vichwa, nitapigia kura sekta ya afya inayothamini maisha, nitapigia kura maendeleo yanajali utunzwaji wa mazingira, nitapigia kura uwazi wa serikali, nitapigia kura uwajibikaji wa kibajeti, nitapigia kura uhuru wa mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali, nitapiga kura kukataa siasa za hadaa na propaganda mfu, nitapigia kura amani ya kweli kwa wote, nitapigia kura vyombo vya dola kutotumika kukandamiza, nitapiga kura kuonyesha nachukizwa na vitendo vya kihuni vya vyombo vya utawala, nitapigia kura maendeleo ya kweli.