Mawazo chanya kwa watafutaji

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
KUNA msemo wa Kiingereza usemao, "Hakuna mtu mwenye tatizo la fedha, bali tatizo ni kukosa wazo litakalomuwezesha kupata fedha.."

Hilo ndilo linaitwa wazo la biashara. Ni ukweli ulio bayana kuwa tatizo la fedha linasababishwa na mfanyabiashara mwenyewe kutokuwa na mawazo, hasa wazo jipya ambalo litakuwezesha kupata fedha.

Ni muhimu kujenga uwezo wako wa kufikiri kiubunifu, kutafuta mawazo na kugeuza mawazo yako kuwa biashara na kufanya kuwa ndiyo kila kitu katika maisha yako yote utakayoishi hapa duniani, ndipo utakuwa na sifa ya kuitwa mjasiriamali.

Mtu ambaye hana mawazo ya fedha, hawezi kuendelea kwa kuwa anawaza kufanya kazi za kuajiriwa tu siku zote lakini si kuwa muanzilishi wa biashara mpya au kampuni yake yeye mwenyewe.

Vilevile mfanyabiashara wa jinsi hii hata ukimpa milioni kadhaa leo hii kwa ajili ya mkopo au mtaji wa biashara, pesa hizo haziwezi kumsaidia kwa kuwa amekosa ubunifu wa vitu vipya ambavyo vitamuingizia pesa.

Kwa kuwa wafanyabiashara walio wengi ni wavivu katika kubuni biashara mpya, kuna wengine wakipata fedha ndiyo hufikiria cha kufanya badala ya kufikiri na kubuni biashara mpya wakati wanajua kabisa wanataraji kupata pesa ambazo watafanyia biashara.

Tusifiri kwamba wawekezaji wakubwa walipokuja nchini walikuja na pesa, lah hasha! Wao walikuja na wazo jipya…kwa nini mfanyabiashara wa leo unatanguliza pesa mbele badala la wazo jipya katika biashara yako? Tubadilike ili tufikie malengo.

Wafanyabiashara wenye upeo mpana kwenye kufikiri walipoona kuwa mawazo yao ni sahihi kibiashara, waliandaa michanganua ya biashara na kisha wakaenda benki na kwenye taasisi mbalimbali kuomba mitaji au mikopo, hatimaye walianzisha biashara pamoja na kampuni zao ambazo mpaka leo zinafanya vizuri.

Hivi ulishawahi kujiuliza, wabunifu, waanzilishi pamoja na wamiliki wa makampuni makubwa kama vile Vodacom, Precision, TBL n.k hapa Tanzania wana pesa kiasi gani? Je unafikiri walianza na pesa ?….ila mawazo yao yalikuwa sahihi kwa kuwa na fikra endelevu za kubuni kwa kuwa na mawazo mapya ya biashara.

Ifike mahali wafanyabiashara wawe na mawazo yafaayo kibiashara lakini pia ukiwa na pesa bila wazo kamwe haitakusaidia kukua kiuchumi. Wengi watajiuliza wazo jipya la biashara ni lipi? Jibu ni kwamba lile lenye kuhimili ushindani ikilinganishwa na biashara zingine na uwezo wa kiushindani unaweza kuwa ni ubora wa bidhaa au huduma, bei, mkakati wa mauzo, usambazaji pamoja na upatikanaji wake.

Kwa mtazamo wangu ni vizuri kwa mfanyabiashara kukuza uwezo wako wa kubuni biashara kwa kupata elimu rasmi, kutokujifanya maskini jeuri na pia kuangalia manufaa linganishi kwa maana ya ushindani uliopo kati yako wewe na wafanyabiashara wenzako.

SOURCE: NI vizuri mfanyabiashara kubuni wazo jipya la biashara

Edna Bondo
Tanzania Daima
19 juni 2012
 
kati ya siku nilipita JF kwa faida ni leo nimejifunza kumbe sasa ni wakati mzuri wa mimi kubuni wazo jipya la kibiashara shukrani sana
 
Nitawezaje kubuni wazo la biashara ilhali sina mtaji na sina dhamana ya kuchukua mkopo bank?? Nijuze hapo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…