Mawazo Haya Yatatusaidia Katika Elimu Yetu ya Sekondari......

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
409
Reaction score
31
Wakuu,

Wakati tukisubiri ripoti ya Tume ya Profesa Sifuni Mchome inayochunguza sababu ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2012 kufeli sana katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha nne, naomba nipendekeze yafuatayo:-

1. Wanafunzi watakaokuwa wakifaulu mitihani ya kumaliza darasa la saba ambao watapata angalau alama 160 kati ya 250, Serikali iwasamehe kulipa ada na michango ya kidato cha kwanza pindi wajiungapo na elimu ya Sekondari katika shule za Serikali.

2. Kila mwanafunzi wa Sekondari ambaye ataamua kuchukua masomo ya Sayansi angiapo kidato cha tatu, asamehewe kulipa ada kwa sharti kuwa wastani katika masomo yake ya kidato cha tatu na nne usiwe chini ya maksi 41. Iwapo atapata wastani chini ya 41 lakini zaidi ya maksi 30 alipe nusu ada. Na iwapo wastani wake utakuwa chini ya maksi 30 inashauriwa alipe ada kamili pamoja na kwamba atakuwa anachukua masomo ya Sayansi.

3. Kwa Wanafunzi ambao watakuwa hawachukui masomo ya Sayansi nao wasamehewe kulipa ada mwaka unaofuata iwapo wastani wao katika mwaka uliopita utakuwa si chini ya maksi 41 katika masomo yao.

4. Wanafunzi wote ambao wastani wao katika masomo yao ya kumaliza kidato cha tatu utakuwa si chini ya maksi 41, Serikali iwasamehe kulipa ada kwa ajili ya kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne ambayo hulipwa NECTA.

Jioni njema kwenu wote.
 

Mimi nashauri Serikali IONDOWE ada kuanzia chekechea mpaka Chuo Kikuu!
 
Kijakazi,

Ushauri wako ni mzuri. Ila kwa jinsi serikali yetu inavyoendesha mambo yake ni bora ada hizo ziendelee kuwepo ila serikali kuu ndiyo iwajibike kuwalipia wanafunzi kwa kupeleka malipo ya ada husika katika shule zetu.
 
 
Ushauri ni Mzuri, Ila tatizo wanafunzi wenyewe, wengi wao hicho kitu kwao sio motisha. Wengi hawajui wamefuata nini huko shuleni.Hiyo ni motisha kwa wazazi.

Sana sana labda useme wanafunzi watakaofaulu vizuri tutawaletea Msanii Diamond. Kwa hilo wengi watakaza buti.
 

Ni kweli vijana wetu wengi hawatilii maanani sana umuhimu wa wao kuwa shule na utumiaji muda wao wa shule. Pia ni bahati mbaya sana kama taifa hatuna mpango mkakati wa kuwajenga vijana wetu na kuhakikisha kuwa wanajituma ipasavyo katika masomo yao. Kuna haja ya kuacha kuendelea kuwalaumu vijana wetu bali tuwasaidie kuwaongoza katika elimu yao na maisha yao kwa ujumla ili watimize ndoto zao maishani kwa faida yao na taifa letu na vizazi vijavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…