Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Hakuna taifa lolote lililoendelea pasipo maaarifa. Huu ni ukweli ambao wengi wetu hatupendi kuusikia. Mataifa ambayo kwa sasa yako juu yote ni mataifa ambayo yamehangaika kutafuta maarifa na kuyakusanya kwa miaka mingi sana. Haya maarifa ndio yanawafanya waendelee kila kukicha. Tunahitaji kufunguliwa akili zetu ili tuweze kupata maarifa. Maarifa ni kitu chema sana ila utafutaji wake ni mgumu lakini madhara ya kutokuwa na maarifa ni makubwa zaidi. Tutaanza kupiga hatua ya kimaendeleo ni pale tutakapoanza kupata maarifa. Maarifa na maendeleo hatuwezi kuvitenganisha hivi vitu viwili ili uendelee lazima uwe na maarifa. Kwahiyo lazima tufikiri kuhusu hili.
Tumefungwa na tunashindwa kuendelea sababu hatuna maarifa, hatuna maarifa kwasababu hatufikiri na wala hatuhangaiki kutafuta maarifa tunasubiri mzungu agundue kitu ili atuuzie, tunapeleka utajiri wa taifa letu katika mataifa mengine na taifa letu linakuwa dhaifu. Taifa lisilokuwa na maarifa ni taifa dhaifu. Kwanza huna uwezo wa kutengeneza silaha zako mwenyewe una nunua silaha kutoka kwa mataifa mengine, na hataweza kukuuzia silaha kali dhidi ya alizonazo utaendelea kuwa maskini kila wakati wa kupokea tu na yeye ataendelea kugundua na kutoa silaha kali na kuendelea kukuuzia matoleo ya chini. Huu ni ujinga kwanini tusijitolee kutafuta maarifa na kutengeneza vitu vyetu wenyewe?
Ngoja niwaambie mataifa mengine yatatuogopa pale tu tutakapokuwa na uwezo wa kutengeneza na kugundua, pale tutakapokuwa na maarifa. Mataifa yenye watu wenye maarifa huogopwa. Wazungu hawapendi tupate maarifa na hawatopenda kwasababu tukiwa na maarifa watashindwa kututawala. Wanaweza hata kuharibu mifumo yetu ya elinmu kwa makusudi wakijua sisi ni watu wenye kujitambua, Wakigundua sisi ni watu ambao tunataka kujitegemea. Hawapendi kuona tukijitegemea watakosa soko la bidhaa zao lakini pia watakosa malighafi. Tuna uwezo wa kuzalisha na kutumia kile tunachozalisha. Tuna uwezo wa kujenga uchumi wetu ukawa mkubwa kama tutawekeza katika maarifa. Ni ni lazima tutengeneze bidhaa zetu wenyewe. Ni lazima tujenge taifa lenye heshima na akili. Taifa lenye maarifa ni lenye kuogopwa. Kwanini tusiwe na hamu ya kuwa na maarifa?
Utandawazi isiwe chanzo cha kuacha kujitambua kama taifa, cha kuacha nia yetu ya kuwa taifa linalojitegemea. Utandawazi isiwe chanzo cha kukana utaifa wetu; ni lazima tujitambue. Sisi sio wamarekani wala wa china ni watanzania. Ni lazima tuwe na dhamira kama watanzania ya kutaka kuendelea na kujitegemea. Kwahiyo taifa letu lazima likue kutaka ndani kuelekea nje na hatutaweza kukua kama hatutaweza kujilinda na kuruhusu ukuaji wa ndani. Kwahiyo lazima soko letu lilindwe. Na kufunza watu wetu katika uzalendo na nidhamu. Tabia za ubinafsi lazima tuziue kama tunataka kuendelea na tujenge jamii ya watu ambao wanataka kutumikia.
Kwahiyo National consciousness ni muhimu sana katika ukuaji wetu kama taifa. Ni lazima tujenge taifa la watu ambao wanajitambua. Ni lazima watu wajiue kuna kitu ambacho kimetuunganisha ambacho ni taifa letu. Na jitihada zetu za pamoja ndio zitakazofanya taifa hili liendelee. Hili sio taifa ambalo group moja linakaa na kwenye madaraka linatawala na kukandamiza wengine. Tunatakiwa tujenge taifa ambalo uhuru wa watu utaheshimiwa. Hatuhitaji watu ambao wanaenda madarakani kwa faida binafsi. Ni lazima tujenge kujitambua huku kwa taifa letu. Kwahiyo akili za watu wetu lazima zielekezwe katika utaifa.
Nimeongelea mara nyingi kuhusu wajibu tatu muhimu kwa taifa lililo bora;
1. Wajibu wa mtu kwa taifa lake.
2. Wajibu wa mtu kwa jamii yake inayomzunguka.
3. Wajibu wa mtu kwa familia yake
Wajibu hizi tatu ni muhimu sana kama tukizitimiza kwa ukamilifu wake. Kwasababu kuna mambo ambayo tunaweza ku solve kama watu binafsi lakini kuna mambo ambayo bila jamii hauwezi kuyatatua kwahiyo tunawajibika kwa jamii. Tunawajibika kwa taifa. Ulinzi na usalama wa nchi yetu unatutegemea sisi raia wa nchi hii na hatutaweza kuendelea kama hakuna usalama wa kutosha. Kwahiyo ni lazima tuache mawazo na matendo ya ubinafsi ambayo yana mong'onyoa jamii yetu, tujenge utaifa. Kwahiyo kujitambua kwetu kama watanzania kuliko kitu kingine chochote ni muhimu. Sisi sio wamarekani, wala wachina wala wajapan sisi ni watanzania. So we must build this National spirit. Hatuwezi kuendelea bila kujitambua huku.
Tunataifa ambalo halijitambui watu wanagombea uongozi kwa maslahi binafsi, hakuna uzalendo. Watoto hawafundishwi kuhusu utaifa. Malezi ya watoto wetu kuhusu utaifa yametetereka. This spirit must return. Lakini katika njia ambayo ni bora zaidi na yenye akili. Kazi inatakiwa ifanyike kurudisha utaifa.
Lakini lazima tutambue pasipo maarifa hatutaweza kufika popote kama taifa. Lazima tufunze watu wetu kupenda maarifa kama maarifa. Na lazima watu wajue maarifa hayana mwisho watu wetu kila siku lazima wawekeze kwenye kujifunza. Ukimaliza chuo sio mwisho wa kujifunza. Mwisho wa elimu sio kupata kazi. Bali kutafuta maarifa na kuyatumia vyema kwa faida ya umma na jamii iliyokuzunguka na kwa taifa na kukuwezesha kuishi maisha bora na yasiyo na madhara. Lakini wengi wetu tunasoma ili kupata kazi na tunafundishwa hivyo hatusomi kutafuta maarifa kama maarifa na ndio maana mitihani tunaiba. Mtu anayesoma kutafuta maarifa hawezi kuiba mtihani huko ni kujidanganya, tunasoma kutafuta uelewa wa mambo yanayotusumbua katika maisha na kutatua changamoto zinazotukabili. Na hili kwa kiasi kikubwa tumeshindwa kama taifa. Mfumo wetu wa elimu umezalisha watu mafisadi na wezi ambao badala ya kutumikia umma na kutatua changamoto zilizopo wanaiba na hiyo sio elimu. Suala la nidhamu na maadili nimelizungumzia mara kwa mara na umuhimu wake nisingependa kulirudia tena lakini ni muhimu sana.