The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
Unaweza kutengeneza maisha yenye furaha ajabu, au maisha yenye sababu nyingi kwanini, hili au lile haliwezekani kwako.
Kuwa mwangalifu na maneno unayozungumza, kwako na kwa wengine. Fahamu mambo unayoamini kuhusu wewe na kuamini ndiyo uhalisia ulivyo.
Kila unachoamini, ulianza kuamini hivyo ukiwa mdogo au, umeamini hivyo ukiwa mkubwa.
Kila unachoamini ni msimamo tu juu ya uelewa wako wa maisha, na ukweli wako, (vile unavyoamini kiuhalisia wako kuhusu mambo mbalimbali).
Kile unachoamini na kujiambia, kiroho au kimwili ni maagizo unayoupa moyo wako ili yatokee maishani mwako.
Unatakiwa kuchunguza kila unachoamini, hasa kile kisichokupa faida.
Usisukumwe na dunia kuamini bila faida. Ni sawa na kuenenda bila akili.
Kila Imani ni wazo lisilofanya chochote.
Kila Imani ni nguvu isiyotokea kuwa chochote, ni nguvu iliyoganda, unaweza kuibadilisha vyovyote.
Kwani ukiamini unaweza kufanya kitu hapohapo kutokea?.
Au ukiamini utafika sehemu, utajikuta umefika kwa kuamini tu?.
Imani inageuzwa na kuwa halisi, kwa kuanza na Kuwazia, kudhamiria, kusema na kisha kutenda.
Sehemu ya maneno ya kujiambia, ukisha kujiwazia na kudhamiria ni. . . .
Unastahili, unaweza, mambo mengi yanawezekana kwako, unaweza zaidi ya unavyofikilia sasa.
Hii huitwa imani kubwa Uwezo mdogo.
Hivyo usijali wewe ni nani una hali gani unatoka wapi, we Jenga hali ya kufurahia kila kitu, maudhi, manyanyaso, na kila kinachosemwa, na vile jamii inakuchukulia vyote viache vipite.
Ni sehemu ya maoni yao na mstari wa kuchora walio uweka kwako.
Wao sio Mungu ila dhamira na imani yako ndiyo Mungu mwenyewe, na ndiye anajua mipaka yako, iliyowekwa na Muumba.
( Sijakosea kusema dhamira na imani yako ndiye Mungu ...) wakati mwingine nitakuletea kwa nini Mungu ni mmoja ila nafsi tatu.
Unastahili nini?
Unaweza nini?
Unafurahia nini?
Kama ni kiroho basi unastahili kuingia Mbinguni. Kama ni mafanikio kimaisha, unastahili kula mema ya nchi kwa kutawala rasilimali za Dunia ikiwemo fedha, mali, familia n.k.
Mungu hakupi unachotaka ila anakupa unachostahili.
Yaani kakuleta uwe askari wewe unataka uwe daktari.
Matokeo yake utawaendesha wagonjwa kama mateka.
Sababu ndani yako una uwezo wa kutumia nguvu na sheria za kuamrisha.
Utakuwa hivyo sababu unachofanya huwezi. Unaweza kile ambacho ndilo kusudio la Mungu la kukuleta ulifanye, Utalipenda.
Na ndilo litakufanya uwe na furaha. Na ndilo, litakufanya ufanikiwe katika hii Dunia.
Uwezo wa kufanikiwa umefichwa katika kipawa chako.
Zile sauti za kukutaka ufanye kitu au shughuli fulani Moyoni mwako, Ndiyo sauti ya Roho wako kukukumbusha asili yako nini, na wewe ni nani.
Hiyo sauti ndiyo, Mungu wako, ndiyo imani yako na ndiyo dini yako kiroho.
Dini za Dunia ni mifumo tu ya kukusaidia kuelewa upande wa pili wa dunia. Ulimwengu wa Kiroho ambako ndiyo kuna asili yako, ndiyo kuna nakala yako halisi. Nakala yenye kila kitu kuhusu wewe.
Mwili huu wa nyama, ni nakala Bandia ya wewe, ( copy ).
Ni kifaa cha kidunia kinachokusaidia kutenda yale yaliyo katika nakala halisi ya kiroho.
Kitamathali.
Wewe ni msanii, na unaishi katika mazingira ambayo ndiyo sanaa yako.
Ni msanii wa kile unachokipenda, unachofurahia, na unachovutiwa kufanya.
Hicho ndiyo sanaa yako. unatakiwa kukifanya, kukiishi ili ufurahie hicho.
Siri nyuma ya sanaa yako ni kufanya kwa raha zako, kisha watu watalipa gharama za furaha yako.
mfano: Zuchu anaimba na kucheza kwa raha zake. Wewe unalazimika kulipia raha zake.
Msanii anachora mchoro kwa raha zake, wewe unamlipa kwa kununua hiyo sanaa yake.
Mwanasiasa anakosoa serikali kwa raha zake. Wewe unamlipa kwa kumpa nafasi.
Ikiwa na maana wote Duniani tunalipwa kwa kufanya vitu tunavyovipenda.
Wewe pia fanya unachopendezwa na Moyo wako. Na watu watalipia raha zako.
kama una kipawa cha kuandika, we andika tu. Yupo atakaye vutiwa na maandishi yako atayanunua akayasome.
Kama una kipawa cha kujua Tiba. We Tibu tu kuna mtu atakuitaji na atalipia hicho kipawa chako.
Kama una kipawa cha Kufundisha. We fundisha tu, Yupo atakaye hitaji kufundishwa jambo na atakulipa.
Kikubwa unatimiza kiu ya Moyo wako.
Hata kama huoni chochote, kwa unachofanya ukiamini unatoa bure ulipwi.
We fanya tu ndiyo wema wenyewe. Atakayekulipa ni aliyeweka hisia hizo za kutoa bure ndani yako.
Yesu alitoa huduma bure, leo analipwa kwa sifa, na kuonwa ndiye Mungu.
Mtume Mohamed, alitoa huduma bure, leo anaswaliwa na Waislamu wote.
Na wewe Atakulipa kwa wakati na majira yake. Achelewi wala hawai. Kama utakuwa na subira, utalipwa gafla na kwa namna yake.
Dini yako iwe. Usichoke kuwasemea, na kuwatendea wengine kwa wema.
Na usikumbuke chochote ulichotoa.
Imani yako iwe Msamaha na kusahau.
Amini: utaiona milango ya bahati zako ikifunguka
Asante kwa wanao Comment, like na hata kusambaza, ili ujumbe uwafikie wengi.
Tuwe pamoja.
Kwa ushauri, maoni na mapendekezo nipigie Kwa namba 0744811338.