Mawazo mapya ya biashara ya kufanya kwa mtaji wa Milioni 500

Mawazo mapya ya biashara ya kufanya kwa mtaji wa Milioni 500

Aigle

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
1,540
Reaction score
7,973
Wadau wa biashara tushirkishane mawazo maoya ya kibiashara

Hapa iwe michongo ile ya biashara ukiweka mzigo kama huo unapiga faida kubwa, sio biashara zile za motivation speaker za kusema anza na malapa pea moja then utafungua kiwanda.
 
Kaka/dada nisikilize vizuri

100m kwa kuanzisha biashara na kutaka faida kubwa kwa TANZANIA utapoteza pesa yote,(Najua hujaelewa)

Kupata vibali tu vya biashara utakuta umetoa rushwa 5m(hujaelewa bado)

Wafanyakazi kwa nchi yetu bado sio waaminifu watachangia pakubwa sana kukufilisi halafu wakuache

Usijiingize kwenye biashara na serikali utatumia pesa yako in advance halafu utabaki na LPO za kudai(utazungushwa ofisi zote, bosi akihamishwa umepoteza pesa)

Ni mara 10 uiweke pesa fixed utakua unaweza kuiangalia na kusema nina 100m

Kwenye hiyo 100 no bora ukanunue hata li uwanja la 50m then uliache utauza hata 60m baada ya mwaka

Kama huwezi, chukua 10% ya hiyo ndio fanyia biashara
 
Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mpunga. Njoo Morogoro weka kijiwe nunua mpunga uweke store godowns kadhaa ufanye distribution of risk.

Kaa miezi sita kuanzia January na February pale mchele umepanda bei toa store koboa uza.

Gunia la huku ni debe 10 hadi 11 baadhi. Gharama ya kuhifadhi gunia moja ni 3000. Unanunua gunia hata la 130,000 au hata 140,000. Unaongeza hela ya usafiri, unanunua nyingi unaita powertiller au tractor ibebe gunia 20 hivi 30. Unaweka store ukiliuza pale January halishuki 200,000. Hapo tunafanya hutaki usumbufu wa kutafuta order ya mchele sokoni.

Alternatively, unaweka store mpunga unakoboa sample unaenda nayo kwenye masoko. Ukipata tenda unakuja kukoboa na kusafirisha.

Mwaka huu January/February gunia lilifikia 250,000. Msimu huu sidhani litafika uko ila 200,000 niliyokupa ni bei ya chini sana hata Samia aagize mchele kutoka Thailand bado gunia halitoshuka hadi hapo. Na nimekupa bei ya kuuza gunia, sio kukoboa na kuuza mchele ambapo kuna faida kubwa.

Hints:
1. Hakuna haja ya vibali wala kusajili, unakuwa kama mkulima tu.
2. Hakuna usumbufu mkubwa kama unafanya kazi na watu wenye akili. Unless unafanya na idiots.
3. Biashara ni kuifanya mwenyewe ndio unajua undani wake, ila huwezi enda nje na mahesabu ninayokupa.
4. Msimu huu kuna Mhindi kaharibu biashara ndio ananunua kwa bei kubwa akafanya wakulima wakimbilie kwake. Ila kuna njia ya kumbana.

Muda wangu mchache hapa ningekupa nondo zaidi. Hii biashara haisumbui ila sina muda wa kuifafanua zaidi, kuna biashara kichaa zipo zinajulikana.

Alafu ugomvi wangu na wataka ushauri wa JF ni uleule hamtoi details zenu. Hujasema uko wapi. Kwa 100M I assume unaweza toka enda mkoa wowote.

Self employed, private employer au govt. Haya makundi matatu yana muda tofauti na yana muda tofauti wa kusubiria faida.

Niko site....
 
kama unafanya kazi ni heri uwekeze bot au utt amis au uweke fixed then faida utayopata na maokoto mengine utayopata kazini basi utakuwa unawekeza kwenye real estate hasa hospitality mdogo mdogo.
 
Kaka/dada nisikilize vizuri

100m kwa kuanzisha biashara na kutaka faida kubwa kwa TANZANIA utapoteza pesa yote,(Najua hujaelewa)...
Yeye anaomba ushauri wa kufanya biashara, wewe unaleta ishu za kununua viwanja[emoji56]
 
Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mpunga. Njoo Morogoro weka kijiwe nunua mpunga uweke store godowns kadhaa ufanye distribution of risk...

LMC_07072023_150513.Version 1 not ready.jpg
 
Mkuu umetisha, kumbe unazungumza jambo unalolifahamu vizuri . BIG UP
Huwa mnasingizia biashara ya kuhadithiwa ina matokeo tofauti kumbe mara nyingi mnatafuta ushauri kwa watu hawaijui wanaisikia, walifanya zamani (mfano hii nayosema hapa ukitafuta aliyefanya mwaka jana anakupa projection tofauti na ya sasa, baadae unalalamika), wabongo wengi wako too optimistic wanawaza faida kubwakubwa haraka, kufanya kazi na vilaza, wababaishaji, wapuuzi, matapeli.
Biashara za kuhadithiwa zinaharibiwa na mambo ya ovyo ya Waswahili, haziharibiki kwamba zimefeli. Mambo mengi
 
Mkuu tafuta wilaya moja mkoani ambayo hakuna wakala wapeps,coca ingia mzigoni,Kisha ingia metl agiza vinywaji,ingia bakhresa food product agiza maji,juis aina zote,nenda afya agiza maji,juis aina zote nakuhakikishia utapiga faida ya net profit 4m
 
Idea nzuri hii, ila labda apewe wilaya iwe yake sio baada ya week 2 walete wakala mwingine
Mkuu tafuta wilaya moja mkoani ambayo hakuna wakala wapeps,coca ingia mzigoni,Kisha ingia metl agiza vinywaji,ingia bakhresa food product agiza maji,juis aina zote,nenda afya agiza maji,juis aina zote nakuhakikishia utapiga faida ya net profit 4m
 
Wazo lingine njoo mwanza ujenge nyumba za za kupangisha za 150k kwa mwezi

Nimesema hiyo kwasababu hiyo ni bei vijana wengi wanao anza maisha wanatafuta nyumba nzuri za self one room or two alf kweny markets zilizopo hazkizi mahitaji(low quality)
 
Mkuu tafuta wilaya moja mkoani ambayo hakuna wakala wapeps,coca ingia mzigoni,Kisha ingia metl agiza vinywaji,ingia bakhresa food product agiza maji,juis aina zote,nenda afya agiza maji,juis aina zote nakuhakikishia utapiga faida ya net profit 4m
Motivation speaker mzigoni
 
Back
Top Bottom