Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mpunga. Njoo Morogoro weka kijiwe nunua mpunga uweke store godowns kadhaa ufanye distribution of risk.
Kaa miezi sita kuanzia January na February pale mchele umepanda bei toa store koboa uza.
Gunia la huku ni debe 10 hadi 11 baadhi. Gharama ya kuhifadhi gunia moja ni 3000. Unanunua gunia hata la 130,000 au hata 140,000. Unaongeza hela ya usafiri, unanunua nyingi unaita powertiller au tractor ibebe gunia 20 hivi 30. Unaweka store ukiliuza pale January halishuki 200,000. Hapo tunafanya hutaki usumbufu wa kutafuta order ya mchele sokoni.
Alternatively, unaweka store mpunga unakoboa sample unaenda nayo kwenye masoko. Ukipata tenda unakuja kukoboa na kusafirisha.
Mwaka huu January/February gunia lilifikia 250,000. Msimu huu sidhani litafika uko ila 200,000 niliyokupa ni bei ya chini sana hata Samia aagize mchele kutoka Thailand bado gunia halitoshuka hadi hapo. Na nimekupa bei ya kuuza gunia, sio kukoboa na kuuza mchele ambapo kuna faida kubwa.
Hints:
1. Hakuna haja ya vibali wala kusajili, unakuwa kama mkulima tu.
2. Hakuna usumbufu mkubwa kama unafanya kazi na watu wenye akili. Unless unafanya na idiots.
3. Biashara ni kuifanya mwenyewe ndio unajua undani wake, ila huwezi enda nje na mahesabu ninayokupa.
4. Msimu huu kuna Mhindi kaharibu biashara ndio ananunua kwa bei kubwa akafanya wakulima wakimbilie kwake. Ila kuna njia ya kumbana.
Muda wangu mchache hapa ningekupa nondo zaidi. Hii biashara haisumbui ila sina muda wa kuifafanua zaidi, kuna biashara kichaa zipo zinajulikana.
Alafu ugomvi wangu na wataka ushauri wa JF ni uleule hamtoi details zenu. Hujasema uko wapi. Kwa 100M I assume unaweza toka enda mkoa wowote.
Self employed, private employer au govt. Haya makundi matatu yana muda tofauti na yana muda tofauti wa kusubiria faida.
Niko site....