Mawazo na mbinu za biashara

Haroonricher

Member
Joined
Jan 15, 2020
Posts
37
Reaction score
19
Habarini wanaJF,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 ni mwajiriwa wa serikali na nipo katika ajira kwa miaka 10 sasa. Kutokana na changamoto na kero za ajira niliona kama sijiskii kubaki katika ajira yangu nikiwa natamani kujitegemea. Kwa hali hiyo nikaona njia pekee ya kuwa huru ni kuwa na self employment, yaani nijiajiri.

Nimeweza kuweka viakiba kujikusanya nikapata TSH. 34M (Milioni Thelasini na nne)

Naombeni ushauri wenu
(1) Je, hiki kiwango kinatosha kuamua kujitegemea?
(2) Je, ni biashara gani niifanye?
(3) Nitaweza kufanikiwa kimaisha kwa huo umri wa miaka 32?

Sijawahi kujishughulisha na biashara nyingine zaidi ya ufugaji kuku lakin si sana japo uzoefu ninao.. Msaada wa ushauri tafadhali.

Ushauri wako mzuri kwangu ndiyo pona pona yangu.
Mungu awabariki.
ASANTE
 
Mkuu sio lazima ufanye kitu unachofahamu pekee, unaweza kfanya tafiti na kuingia kwenye biashara yeyote kikubwa ni taarifa muhimu za hiyo biashara na kujitolea wewe binafsi katika kuhakikisha lengo lako linatimua.

Mfano sikuwa kuwa mkulima ila nimelima hekari 20 za mahindi kikubwa ni kuwa karibu na kazi yako. "watu ni muhimu sana ili ufanikiwe lakini usimuamini mtu yeyote". yangu ni hayo
 
Mkuu hiyo ni kubwa sana Mimi nikipata milioni 10 tu nimeshatoka, hujasema wewe ni mwenyeji wa wapi ila kama unayo idea ya biashara ya nguo hapa Mwanza inalipa. Cha kufanya wewe tafuta frame pale pamba road town then ungana na wale wafanyabiashara wanaoenda kununua mizigo Nairobi hope utafanikiwa. Nimeona watu wengi walianza kama machinga na hawakua na mtaji mkubwa kama wewe but wametoboa na wao sasahivi wanamilika frame hapo mjini.
 

Dadavua kidogo, mwenendo wa biashara na gharama za vitu kama frame maeneo hayo.


Alexander
 
Dadavua kidogo, mwenendo wa biashara na gharama za vitu kama frame maeneo hayo.


Alexander
Frame zipo kuanzia milioni moja na nusu hadi milioni nne kwa mwaka. Ila frame nzuri na kwenye mzunguko mkubwa wa pesa ni hapo pamba road japo maduka ni mengi ila location itakulipa boss.

Biashara iko vizuri lakini pia hii misimu ya sikukuu utapiga pesa sana wateja ni wa jumla na rejareja pamoja na machinga naona wafanyabiashara wengi kutoka katoro, nyehunge kahama na kwingineko wanakuja kuchukua mizigo hapa Mwanza mjini.
 
Mkuu kama imani yako inaruhusu fuga mbuzi katoliki. Hutajuta kama utawashirikisha na madaktari wa mifugo. Mimi sifanyi huo ufugaji ila kwa sasa nakusanya mtaji walau 2M nianze kidogo.

Shughuli nyingine ni kilimo cha parachichi ambacho hicho itakubidi uwe msahimilivu wa walau miaka 3 na kuendelea kwa sababu katika muda huo wewe utakua wa kuhudumia shamba na kulipa vibarua so uvumilivu ni muhimu kabla hujaanza kupata output.

Pia katika kilimo hapohapo jaribu kufanya research kilimo cha alizeti na maharage kitu ambacho ndio nafanyia kazi kwa sasa. While am on my middle twenties hizo ndio shughuli nafikiria kufanya wakati bado najikusanya kusanya.

Regards!
 
Kama upo mikoa kama Mwanza, Arusha...

Usi-Risk pesa zako, katika 34M weka 33.8M Bank, mkononi ubaki na 200,000 Cash then ingia PM kwangu nikueleze mbinu ya kutumia rasilimali watu kupata 300,000 Tzs kwasiku.
 
Hio pesa nyingi kweli yani hapo unachukua kiasi flani unatafuta location unapiga min market yako safi hukosi faida ya elfu 80-laki kwa siku
 
Kwenye kilimo ajipange ila kinacholipa maharage maana ni miezi miwili 2 unavuna.

Fikiria
1.Unalima mwenyewe maharage ukishavuna unajiuzia mwenyewe
2.ukishajiuzia unayapeleka kwenye duka lako la nafaka unauza reja reja aisee mika 5 haukamatiki

Nb๐Ÿ˜›esa ya shamba na duka usichanganye zinajitegemea
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hebu nieleweshe hapo unapojiuzia halafu unapelekea duka la nafaka. Unawauziaje wa maduka ya nafaka kiasi kwamba inaweza kuwa faida zaidi. Nifafanulie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni Nipo Mbeya lakini suala la fursa za biashara hata kama itakuwa ni mkoa wowote mi naifuata hiyo fursa..kwahiyo mwanza siyo mbali ninaweza kwenda nikafanya research kabla sijaachana na ajira yangu ya awali ili nipate pa kuanzia..
By the way Aksante sana kwa mawazo kaka aksante sana๐Ÿ™๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿพ
Shukrani sana sana mkuu kwa ushauri nitaufanyia kazi..pia kama kuna mawazo ya ziada naomba kuendelea kunifuatilia ili kunipa hamasa zaidi nifanikishe lengo langu la kujiajiri..Aksante sana mkuu
 
Mkuu biashara ya nafaka haitakuacha vibaya.
Biashara ya nafaka, kwamba niwe na duka la kuuza vyakula au niwe na aina flani tu zao la nafaka ambalo ndilo ntakomaa nalo?? Kwa mfano Mahindi au Maharage au Mchele au nipige vyote mixer mkuu please naomba nielekeze vizuri mana nipo Mbeya na nafaka zipo sana
 
Ushauri wangu ni biashara ya Nafaka hasa mkoa wa MTWARA kule nimeishi sana tu. hawalimi mazao ya chakula hivyo kuna uhitaji mkubwa wa nafaka hasa maharage, mchele, unga (mahind). Usiache kazi mapema. Chukua mil. 15 tu ingia shambani nunua mchele peleka kule nakuhakikishia utatoboa haraka sana. Fremu kule ni bei ndogo tu.

Hakuna wizi mostly watu wa kule ni wastaarabu na wakarimu hawana zile kusema mgeni wasinunue hapana. Nilifurahi sana kuwa kule. Mimi pia nitazama huko kufanya biashara za nafaka . Usiogope ugeni.

Biashara kule ni safi kabisa bei nzuri pia. Sio walalamikaji wa bei wenyewe wamezoea bei ghali karibia kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ