Mawazo na mbinu za biashara

Imani inaruhusi mkuu, Wazo lako nimelipokea nalifanyia kazi na pale nikihitaji muongozo mkuu nitakutafuta..leongo ni kuhakikisha kwa umri nilionao nisije nikajiingiza sehem nikapotea mazima
 
Ni ushauri mzuri sana mkuu nitaufanyia kazi isipokuwa labda ungenishauri zaidi juu ya kuacha kazi au kutoacha mapema maana nipo mkoa wa Mbeya sasa kwa hii biashara ya kusafirisha mazao inamaana kwamba nimpe mtu anifanyie kazi kwasababu kazi ninayoifanya hainiruhusi kumove hovyo na hata nikitoka siwezi kaa mda mrefu...
Lakin ushauri mzuri sana
 
Naomba ufafanuzi kidogo hapa mkuu tafadhali
 
Naomba ufafanuzi mkuu ili nipate idea mana ni jambo jipya kwangu hili
Hio pesa nyingi kweli yani hapo unachukua kiasi flani unatafuta location unapiga min market yako safi hukosi faida ya elfu 80-laki kwa siku
 
Ndugu tuliza akili sanaaaa.

Chagua moja and focus.

Kuna mdau alikuambia invest kwenye kuku.

I second him/her.

Anza kwenye familiar grounds halafu spread to related businesses.
 
Kama upo mikoa kama Mwanza, Arusha...

Usi-Risk pesa zako, katika 34M weka 33.8M Bank, mkononi ubaki na 200,000 Cash then ingia PM kwangu nikueleze mbinu ya kutumia rasilimali watu kupata 300,000 Tzs kwasiku.
Sawa sawa mkuu nitakuchek unielekeze mkuu..shukrani sana
 
Ndugu tuliza akili sanaaaa.

Chagua moja and focus.

Kuna mdau alikuambia invest kwenye kuku.

I second him/her.

Anza kwenye familiar grounds halafu spread to related businesses.
Ni shughuli ambayo nimeifanya kwa mda kidogo japo ilikuwa ni small scale but kwa ushauri wenu inabidi niangalie kwa mapana zaidi ili isije ikanidodea nikiwa nipo Independent sipo kwenye ajira mkuu..
Aksante kwa ushauri
 
Hofu
Hofu yangu ni vile tu naogopa kurisk pesa kwenye biashara isiyotabirika huku nimeacha kazi..labda nielekeze vizuri
Lakin hili ni wazo zuri mkuu aksante
 
Hofu

Hofu yangu ni vile tu naogopa kurisk pesa kwenye biashara isiyotabirika huku nimeacha kazi..labda nielekeze vizuri
Lakin hili ni wazo zuri mkuu aksante
Sijui niweke namna gani kukusaidia ila kiufupi kadri biashara inavyozidi kutabirika ndivyo inavyopunguza thamani/faida yake. Yaani kwa mfano ukitumia milioni 50 kujenga fremu za kupangisha na kutumia 50 hamsini 50 kupeleka ngombe comoro, hii ya ngombe itakupa faida haraka sababu uwezo wa kupoteza ni mkubwa. Kuna uzi niliusoma humu unasema biashara ni kamari. Ndio maana nikasisitiza muhimu ni kujitolea wewe kupata maarifa ya kile unachotaka kufanya na kukipa first priority. Kingine kujiamini na kufanya kazi kwelikweli
 
Kuacha kazi ni suala la nafsi ningekushauri baada ya kujiridhisha wewe na nafsi yako ndio uchukue hii hatua kwa kuzingatia namna utakavyoendasha maisha ila usijipe sababu ya kujilaumu maana ujasiriamali ni mguu sana
 
Hapa nimekupata uzuri mkuu nadhani kuna ulazima wa kufanya tafiti kwanza kabla ya kufanya Maamuzi ya kuingia. Pia kwakuwa mdau wangu upo hapa nikiwa na shida yà ushauri naomba usisite kunipa na pia mbinu mbali mbali kwani katika biashara kiukweli mimi ni mgeni..
Aksante sana kwa ushauri
 
Ni hivi mfano labda anataka kulima maharage...labda katika kulima kwake ametumia 5M..baada ya kuvuna mteja wa kwanza anakua yeye mwenyewe anajiuzia kwa bei halisi kama vile anavyotaka kuuza kwa wengine kwa bei ya jumla..hapo anakua ameaharudia pesa ya kulima na faida.

Baada ya hapo anayachukua yale mazao anapeleka kwenye duka lake la nafaka napo anauza kwa bei ya reja reja..akipata faida tayari anakua na msingi wa biashara mbili pasipo kuchanganya.
1.Anakua na msingi wa kulima na faida na soko la uhakika kwa sababu mteja wa kwanza wa mazao anayolima ni yeye mwenyewe.
2.Mbili akishajiuzia anakua anapeleka moja kwa moja dukani kwake kuuza kwa bei nafuu..

Hii system hata matajiri wakubwa wanaitumia sana,wanalima wenyewe na wajiuzia wenyewe kabla ya kumfikia mlaji

Nb:Mimi sio mfanya biashara najaribu kucreat idea tu hapo na Maharage ni kitu cha kwanza kukifanyia research Mungu akijaalia nitafanya hiyo biashara.
Mkuu hebu nieleweshe hapo unapojiuzia halafu unapelekea duka la nafaka. Unawauziaje wa maduka ya nafaka kiasi kwamba inaweza kuwa faida zaidi. Nifafanulie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuacha kazi ni suala la nafsi ningekushauri baada ya kujiridhisha wewe na nafsi yako ndio uchukue hii hatua kwa kuzingatia namna utakavyoendasha maisha ila usijipe sababu ya kujilaumu maana ujasiriamali ni mguu sana
Suala la kuachana na kuajiriwa nimelifanyia kazi, nipo tayari kwa lolote isipokuwa tu nahitaji hiki kiasi cha pesa nilichohangaikia kukipata nikitendee haki mkuu..
 
Hapa umeeleweka vyema..ufafanuzi mzuri na ushauri wenye tija..
Aksante sana
 
Anza na Mchele na Maharage ndo kitu ambacho vipo kwenye trend ya maisha yetu kila siku...unaweza ukaongeza nafaka zingine baadae.

Pia kwa mtaji wako jaribu pia uwe unanunua mahindi mikoani kwa bei nafuu(hapa hakikisha umeyapima ili usiuziwe mabichi) kisha saga unga na uza bro nakuhakikishia utatoka hiyo hela nyingi sana na usithubutu kufanya biashara kienyeji.

Kwahiyo boss duka linakua hivi unauza maharage kwa bei ya jumla na reja reja na mchele pia...huku pia unachukua mahindi unakuja kuyasaga na kutengeneza unga.

Nimekupa wazo fanya research ujue ni kiasi gani kitatosha lakini ushauri wa ziada katika hiyo hela usiiingize yote kwenye biashara mfano labda una 25M unaweza ukachukua 10 au 15M ukafanyia biashara na inayobakia unaweka kwa ajili ya dharura.

Nb:Location ni jambo la kuzingati


.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu asante sana kwa hili nadhani ni jambo kubwa umelieleza hata hivyo ni wazo la biashara miongoni mwa mawazo mengine ambalo ntakuwa attached moja kwa moja na jamii...
Ila mkuu unesema kuwa
""na usithubutu kufanya biashara kienyeji""
Hii vipi..
 
Kaka ushauri wangu katika kuacha kazi ni kwamba angalau uwe tayari na kabiashara ambako kanaweza cover expenses zako za kuishi ndio uache kazi.
Kiukweli niliangalia zaidi katika kupata experience ndo mana nikajiingiza kwenye ufugaji mdogo ili nipate japo la kujifunza..lakini pia aina ya ajira niliyonayo hainiruhusu kuwa mbali na mazingira ya kazi japo biashara kama ya duka ningeweza kuwa nayo lakin skufanya hivyo na badala yake nikapambana kupata hicho kiasi cha fedha ili hata nikitoka nikapatie uzoefu na mawazo mapya nikiwa katika motion...hivyo sijajiwekea mazingira ya hofu baada ya kutoka kwenye ajira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…