Mawazo ya biashara na michanganuo yake

Mr Confidential

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,532
Reaction score
2,415
Habari,
Leo naomba tushirikiane katika kuchangia mawazo ya biashara na ujasiliamali pamoja na michanganuo ya gharama. Hapa lipatikane jibu la swali hili ""Nina laki 2, laki 5, milioni 1, milioni 5 nk nifanye biashara gani?""

Kwa kuanza nitatoa mchanganuo wa kilimo cha machungwa ambacho ni maarufu sana katika mkoa wa Tanga, Pwani, Morogoro nk

*Ununuzi wa shamba (pori ) ekari 10. @100,000. Jumla ni 1, 000, 000 kwa maeneo ya mkoa wa Pwani.

*Kukata miti na kung'oa visiki. Ekari 10 @50,000. Jumla ni 500, 000

*Kulima ekari 10 kwa trekta. @60,000. Jumla ni 600, 000

*Upimaji ili kupiga mashimo yalinyooka ekari kumi. Kwa ekari 10 jumla ni 200, 000 yaani kila ekari ni 20, 000.

*Upigaji wa mashimo ya kupanda miche Kwa ekari 10 mashimo yatakua 1400. Urefu kutoka shimo hadi shimo ni mita 6. Hivyo 1400×500=700, 000

*miche 1400 jumla ni 420, 000. Yaani kila mche ni tshs 300.

*kupanda miche ekari 10. @10,000 jumla ni 100, 000.

Jumla kuu ni 3, 520, 000 (Milioni tatu, laki tano na ishirini elfu) Ila kadiria kama Milioni nne (4, 000, 000)

Msimamizi ni wewe mwenyewe.

Karibuni

Mr Confidential
 
Usha achana na wazo la ufugaji wa kuku na sasa uko kwenye Machungwa?
 
Tunatakiwa tuingie field wakuu...baada ya kufanikiwa ndio tulete mrejesho;tofauti na hapo,mipango mingi ya makaratasi huwa inaridhisha na kuvutia sana.
 
Hesabu yako kwenye kung'oa visiki haikk sawa... umeandika 5,000,000/=
 
Na ukishapanda miche inachukua muda gani hadi kukua na kuanza kuzaa machungwa?
 
Na ukishapanda miche inachukua muda gani hadi kukua na kuanza kuzaa machungwa?
Miaka mitatu hadi minne. Mchungwa hukaa zaidi ya miaka 40, kuvuna ni mara mbili kwa mwaka. Kazi yako itakua ni kipalilia shamba na kupruni tu
 
Miaka mitatu hadi minne. Mchungwa hukaa zaidi ya miaka 40, kuvuna ni mara mbili kwa mwaka. Kazi yako itakua ni kipalilia shamba na kupruni tu
Duuh Kama ni kweli hvyo Basi ni Business nzuri ukilinganisha na yale mazao ya kulima Tena kila mwaka.
Vipi kwa maeneo ya Dar es salaam na pwani hyo inawezekana?
 
Duuh Kama ni kweli hvyo Basi ni Business nzuri ukilinganisha na yale mazao ya kulima Tena kila mwaka.
Vipi kwa maeneo ya Dar es salaam na pwani hyo inawezekana?
Kwa Dar sina uzoefu wowote, lakini kwa pwani inawezekana
 
Mimi nimemuelewa anachotaka kusema.
Amemaanisha hivi machungwa yakishakomaa na kuiva inachukua muda gani kuanza kuyavuna mpaka yaishe shambani?
Yaani as long as mchungwa upo mavuno yao, Ni kama maembe. Kwa mwaka machungwa yanavunwa mara mbili, February na September. Mchungwa unaweza kuishi zaidi ya miaka 40.

Kwenye shamba la Mzee wangu kuna michungwa uliyopandwa mwaka 1990 na bado ipo imara.

Mchungwa wenye miaka sita na kuendelea huweza kutoa machungwa karibu 800 au zaidi. Kuna michungwa shambani kwa mzee huzaa machungwa zaidi ya 2000.

Kama upo kwa dhamira ya kumake quick money kilimo hiki hakikufai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…