KYAMTUNDU
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 1,820
- 295
Ndugu zangu, nimekuwa niwasikiliza sana watanzania wenzetu hasa wale makada, wanachama, mashabiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu idadi ya watu waliotoa maoni kwenye Tume ya Kukusanya Maoni iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba. Watanzania wenzetu hawa wamekuwa wakielekeza utii wao kwenye IDADI ya watanzania waliotoa maoni kuhusu uhitaji wa serikali (siyo nchi) tatu. Na sababu kubwa za kupendekeza muundo huo zimeoneshwa kwenye Viambatanisho vya Tume uk.248-249 Hoja yao kubwa ni kwamba wananchi sawa na asilimia 15% ya watanzania 323, 001 waliotoa maoni HAWAWEZI kuwa wawakilishi wa MAONI ya wananchi-ni idadi ndogo! Sasa naomba makada hawa walioishiwa hoja wajibu maswali yafuatayo: 1. Je, ni halali wajumbe 630 (0.000014% ya watanzania wote ) wa Bunge la Katiba kufanya uamuzi kwa niaba ya watanzania 44, 928,923 (NBS:2013) na mawazo yao yakakubaliwa?!
2. Je, ni halali kwa Jakaya Mrisho Kikwete aliyepata kura 5, 276,827 (0.24% ya watu milioni 22 waliojiandikisha mwaka 2010) kuwa Rais halali aliyechaguliwa na wananchi?
Sasa CCM wameongeza upuuzi kwa kuyagawa maoni hayo kwa kigezo cha mahali maoni hayo yalikotolewa. Leo katika kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV, nimemsikia KADA maarufu (japo anaonekana anatumia sana nguvu badala ya hoja) Christopher Ole Sendeka akisema Maoni ya kutaka serikali tatu yalitolewa Kigoma, na Pemba! CCM wanaopinga kuigawa nchi katika serikali tatu, wanaona ni heshima kuyagawa maoni kwa kuangalia mahali yalikotoka! Huu ni upuuzi. Hata hivyo nimeona ni vyema kuelekeza maswali yafuatayo kwa wenzetu wa CCM:
1. Je, ni halali kwa Dk. Mohamed Shein kuwa Rais halali wa Zanzibar wakati asilimia kubwa ya kura zake 179,809 (ZEC 2010) zilitoka Unguja?
2. Dk. Shein ni Rais wa Zanzibar au Rais wa Unguja?!
CCM walete hoja, wasifiche vichwa na kuacha viwiliwili nje.