Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
"Upendo upo ili tulindane", Kichwamaji, E. Kezilahabi
MAHUSIANO.
Tukiacha kufikiri kifalsafa, mapenzi ni kama rangi ya urembo kwenye haya maisha yetu. Na mara nyingi kupitia upendo uliozaliwa na mahusiano, tunapata maana ya maisha ndanimwe.
Mahusiano yanamuhusu kila mtu, hii ni mada pendwa na wengi ambao wapo au wanatarajia kuingia kwenye mahusiano. Kezilahabi ameweka mawazo yake kuhusu mahusiano pia.
Ni vitabu vichache vya Kezilahabi vinavyoonyesha mahusiano yenye utulivu, mahusiano ya sampuli hii ameyaonyesha kwenye Mzingile sura ya mwisho. Lakini ieleweke Mzingile ni kitendawili na mahusiano mazuri aliyoyaonyesha mule ni ya fikra na sio mahusiano ya mtu na mtu.
Mahusiano ya mtu na mtu, ambayo yanahusisha jimai. Kwa kiyunani EROS, yameonyesha kujaa usaliti, dharau na kukosa msingi ya uwepo wake. Maana ya mahusiano, ndoa na mapenzi kwa ujumla yamepoteza maana kwa misingi isiyoendana na mapenzi au mahusiano. Usawa, Uhuru, Utandawazi ni kati ya vitu vilivyoharibu msingi wa mahusiano mengi
Katika UHURU kulizaliwa usaliti, Katika USAWA kukazaliwa dharau. Utandawazi ni mzazi wa UASHERATI.
Hii ni sababu ya Kezilahabi kuonyesha zaidi Uasherati, usaliti na dharau katika riwaya nyingi.
Mahusiano yanaweza yakaanza katika msingi wa mzaha, kulipa kisasi, kuonyesha ugangwe nk, lakini ikitambulika maana mbele ya safari, mahusiano husika hudumu. Heshima, uaminifu, upendo ndio nguzo za familia.
Sio tu vijana, bali hata wazee na watawa nao hushiriki mahusiano ya mapenzi. Uthabiti wa mahusiano yao unaweza kutiliwa shaka, dhati ya uwepo wa huba haitambuliki sana inapoanzia.
Kwenye kitabu cha Dunia uwanja wa fujo, tunamuona jinsi Vero alivyokuwa anamnyima penzi Denis, huku mwenyewe (Vero) akiwa anagawa penzi kwa wengine, hata walipoingia katika ndoa usaliti uliendelea. Mara baada ya Denis kuona upuuzi wa dhana ya usawa, aliachana na Vero na baadae akaambiwa kuwa hata aliyedhani ni binti yake sio binti yake alisingiziwa tu.
Ndoa imepoteza maana yake. Ameandika
Kichwamaji, ni kitabu kingine cha Kezilahabi chenye visa vingi vya mahusiano, wakuu wanaotumia vyeo vyao kuwarubuni mabinti nk. Kwa kuwa anajua uasherati unapendwa, Kazimoto aliona aoe mapema kabla ya kuenda kufundisha ili asijikute amejima wanafunzi wake.
Mahusiano yanaweza kuwa na mwanzo wowote, Kazimoto alianzisha mahusiano kama kisasi lakini akajikuta ametumbukia kwenye mapenzi ya kweli. Lakini katika ujana, uasherati umekuwa ndio ada ya vijana waliowengi kwa kukosa muongozo.
Kezilahabi anaona upuuzi mwingi kwenye mahusiano, mapenzi na uasherati lakini picha anayotumia ni kuwa yeye anapenda na ni fundi katika mambo hayo.
Madhara ya mahusiano yasiyo na msingi wa kuanzisha familia yapo katika kitabu cha ROSA MISTIKA, kinachofanya mwanamke ahame mji ili akaolewe na mtu asiyefahamu historia ya makuzi yake, ili kuepusha mengi. Kama ambavyo wengi walivyomuona Roza kuwa love laboratory.
Gamba la nyoka, utona mahusiano ya padri madevu na mama Tinda. Yote hii ni kusema mahusiano yanauhitaji mkubwa kwa kiumbe na ukiyapinga unaweza kuangukia kwenye unafiki, ukiyaendekeza unaangukia kwenye uzinzi au uasherati.
Kinachomsumbua mwanadamu ni kubalance hisia, mihemko na ufahamu. Je ni sahihi kufuata hisia? Mara nyingi mambo haya huharibu maisha, familia nk dada yake Kazimoto alifariki siku ya kujifungua baada ya kuona malengo yake yalivyopeperushwa baada ya kupata mimba, mama yake alifariki na mwanae kwa kuwa ndio lilikuwa tegemeo lake, wazo lililomfanya naye alipize kisasi.
Wapo wengi wasio na furaha kutokana na mahusiano yalianzishwa katika msingi usio imara kisha mahusiano yakamaanisha ngono.
Kwenye Nagona, aliwauliza kama mnafahamu mfalme Oedipus, alisema "inasemekana tangu atokee, uasherati umekuwa dira ya kufikiri kwenu" Hii hatuwezi kusema kuwa ni dongo kwa Sigmud Freud, ambaye alijikita zaidi katika mahusiano na ngono hata akatoa ile mnaita OEDIPUS COMPLEX, bali ni kizazi chote kwa ujumla