anjo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2009
- 299
- 97
Wanajamii,
Watu wamekuwa wakitoa mawazo yao kuhusu aina ya serikali itakayotuongoza kwa miaka kadhaa ijayo. Watu wametoa maoni ya serikali moja (Tanzania bila ya bara au Zanzibar), mbili (Kama ilivyo kwa sasa) na pia tatu (muungano, Tanzania bara na Zanzibar).
Nimejiuliza ni kwa nini watu kama Walioba, Salim, Butiku na wenzao kwenye kamati ya kuunda katiba wanaweza kusaliti asili yao kutokana na kuanzisha na kukulia ndani ya mfumo uliopo sasa. Kuna analyst alinieleza maneno yanayoelekea kuwa ya kweli kuhusu hii hali:
Itakuwa ngumu kupata serikali moja bila kupitia serikali tatu.
Hii ina maana sana. Kwa sasa, Zanzibar haiwezi kukubali kuitosa serikali ya mapinduzi kutokana na ulaji kwa viongozi na pili kutoelewa kwa wananchi. Kwa upande wa bara, hamna tatizo kwani serikali ya Zanzibar ni mzigo!
Kwa serikali tatu, inaonekana itakubalika zaidi na Wazanzibari wataikubali. Baada ya miaka kadhaa (labda 10 au 15) watu watakuwa wamepata uelewa na kugundua kuwa serikali tatu ni mzigo kwa watanzania hivyo wataweka shinikizo kwa serikali ya muungano kuondoa serikali mbili (yaani tanganyika na Zanzibar) na kubaki na serikali moja ya muungano. Hapa malalamiko yatakuwa machache (labda kutoka kwa viongozi) kutokana na kwamba wote watapoteza tofauti na sasa kwa Zanzibar kuogopa kupoteza serikali ya mapinduzi.
Uchambuzi huu una ukweli zaidi kutokana na kuwepo watajwa hapo juu kuwepo kwenye kamati ya katiba.
Anjo