Mawazo yangu nilipokaa kwenye kiti usiku kutafakari

Mawazo yangu nilipokaa kwenye kiti usiku kutafakari

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Elimu na ujengaji wa tabia tunaweza kuvitenganisha vitu hivi viwili?
kwanini tunaenda shule kama tabia zetu hazito imarika na kutenda vyema zaidi?
Kwanini tunaenda shule kama elimu yetu haitotufanya kuwa wenye faida kwa taifa letu?
Je elimu na ujengaji wa tabia tunaweza kuvitenganisha hivi vitu? Je Tunaweza kwenda mbele kama taifa pasipo tabia zetu kuwa bora?

Kuna adui yeyote ambaye anayetufanya tusiendelee zaidi yetu sisi wenyewe?

Je tunaweza kumuandaa mtumishi wa umma bila kuandaa tabia yake toka yuko shule?

Tunategemea mtu awe na tabia njema pasipo kumjenga katika ngazi ya awali na tunafikiri atatenda katika ukamilifu?

Rudi weka mgongo wako kwenye kiti na kufikiri.

Ni nini baadae ya taifa letu? Je si kweli kwamba taifa hili litajengwa na thoughtful people na bila hao hatutaweza imarika? Sio kweli kwamba misingi imara ya taifa hujengwa katika akili za watu na kutengeneza tabia zao ambazo zitakuwa na manufaa kwa taifa?

Ni kipi unapendwa kuitwa mwenye manufaa kwa taifa au mbinafsi? Ni kipi chenye heshima? Nchi ya wenye bidii au nchi ya wazembe? Naomba tuipime bidii yetu kama taifa je tumewahi hata kufikiri kujaribu kuwa taifa kubwa? Kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wetu?. Je Elimu na tabia za watu wetu sio muhimu kwenye ujenzi wa taifa imara?

Elimu yetu na tabia za watu wetu lazima zijengwe katika fikra za wapi tunataka kwenda kama taifa. Hatuko taifa kuondoa umaskini tuko taifa ili kufanya taifa hili kuwa kubwa that is ''idea'' umaskini utasombwa humu kwa humo kama mafuriko yanavyosomba vitu, lakini bidii yetu lazima iwe kwenye kujenga taifa kubwa. Serikali ambayo iko tu kwaajili ya kuondoa umaskini ni serikali ambayo haina vision. Vision ni kuwa taifa kubwa. Umskini utaondoka wakati tukifuata vision hiyo. Taifa kubwa haliji kwa bahati mbaya ni conscious effort and dedication.

Elimu ni muhimu kwa ukuaji wa taifa lolote, bila elimu hatutafika popote. knowledge is the power. Jamii isiyokuwa na maarifa ni jamii ambayo itatawaliwa milele. Tulitawaliwa kwasababu tulikuwa wajinga hatuna maarifa. Tungekuwa na maarifa wasingetutawala. Tungekuwa na akili wasingetutawala. Huwezi kumtawala mtu mwenye akili. Atakupiga. Tatizo letu hadi leo hii hatutaki kuamka. Na elimu na tabia zetu ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa imara. Hatuwezi kufika tunapotaka kwenda kama hatuna elimu ya kutufikisha huko.

Elimu na tabia za watu wetu zinatakiwa ziangaliwe kwa jicho moja bila ulegelege. Kwahiyo ni lazima tuangalie tabia za watu wetu Tangia wadogo ambapo tutakuwa na wakati mzuri wa kuwanyoosha tunavyotaka. Ni lazima tuwe na wazazi na walimu pamoja na jamii ambayo iko very strictly kwenye moral behavior za watoto wakati wanakuwa, bila ya hivyo tusitegemee viongozi wazuri au kuondoa ufisadi angalau kwa asilimia ndogo. Tusitegemee vigor of the mind which is essential for development. Hatuwezi kuendelea kama tutakuwa na taifa la watu legelege na wasio na fikra bora. Ni lazima tutambue fikra ndizo ambazo hujenga taifa, fikra bora hujenga taifa bora.

Hatuwezi kujenga taifa la watu ambao wana depraved conduct alafu tukategemea kupata opposite result. This country need a bold leadership. We have the potential to become great nation on the earth. But first we must train our kids and we must change the way we think and behave.

Tunahitaji kiongozi atakayejenga moral behaviour za watu wetu kwa sheria na kwa nguvu ya neno. We need a single minded leadership. We all want to come out of this misery and to enjoy great benefit of being great nation. A self sufficient country. I know we can produce and i know we can be a great nation on the earth. it is just the matter of multiplying our efforts.

Ngoja niwaache na maneno slave owner wa huko marekani;

''Let not a ray of light fall on the mental vision of the slave; let him know nothing about christianity but few outward lifeless forms; Make him as stupid and thoughtless as the beast, with no reflection on the past, no care for the future, no sense of wrong, no idea of right, no care of his soul, no knowledge he has one; And in his condition give him enough to eat and drink, and allow him to indulgence of his sensual appetite and all you have a model of perfect slave''

** Tusome vitabu vyao tuchambue na tufikiri wenyewe, tuweke hazina ya maarifa yetu ambayo tumeyahangaikia kwa akili zetu na tuchukue mengine yanayofaa kutoka kwao ili yatusaidie lakini ni lazima tujenge akili zenye kujitegemea kwa watu wetu na sio akili tegemezi. Hatuwezi kuwa huru kama tutakuwa na akili tegemezi. Kila kazi ambayo haikuandikwa na sisi lazima isomwe na kuchambuliwa kwa undani ili kupata maarifa ndani yake tusimeze kila kitu kinachotoka majuu. Kama tutakuwa na hamu ya kujifunza na kutafuta maarifa ili yasaidie taifa letu tutayapata. This country can not grow without morality.
 
Mada nzuri nitarudi baada ya muda kufafanua niliyoandika hapa chini.

Kuna vitu vinavyojenga tabia ya mtu. Vipo vitano (5).

1. Family

2. School

3. Religion

4. Peers

5. Government.
 
Mada nzuri nitarudi baada ya muda kufafanua niliyoandika hapa chini.

Kuna vitu vinavyojenga tabia ya mtu. Vipo vitano (5).

1. Family

2. School

3. Religion

4. Peers

5. Government.

au about genetic makeup?
 
There's a limit where good education can take you.

Education ina mambo mengi pamoja na maarifa ya kazi lakini kuna sehemu nyingine ya kumjenga tabia yake na kumtengeneza uelewa wake ambao utamfanya ahusiane na wengine vyema. Hii tabia inaweza kujengwa wakati akiwa mdogo kwa mafunzo kutoka katika familia na shule. Bila mafunzo haya hatutaweza ku regulate impulses and passion ambazo hu errupt mara kwa mara kwenye young and immature minds. Education plays great role in transforming people and societies. Kwahiyo costant education ni muhimu. Kama tunahitaji kuendelea ni lazima tutengeneze tabia njema kwa watu wetu ambazo zitakuwa chachu ya kuendelea kwetu. Mengine ni siasa tu.
 
Education ina mambo mengi pamoja na maarifa ya kazi lakini kuna sehemu nyingine ya kumjenga tabia yake na kumtengeneza uelewa wake ambao utamfanya ahusiane na wengine vyema. Hii tabia inaweza kujengwa wakati akiwa mdogo kwa mafunzo kutoka katika familia na shule. Bila mafunzo haya hatutaweza ku regulate impulses and passion ambazo hu errupt mara kwa mara kwenye young and immature minds. Education plays great role in transforming people and societies. Kwahiyo costant education ni muhimu. Kama tunahitaji kuendelea ni lazima tutengeneze tabia njema kwa watu wetu ambazo zitakuwa chachu ya kuendelea kwetu. Mengine ni siasa tu.

When I say there's a limit where good education can take you, I didn't imply that education isn't important but rather I was trying say that education can't replace innate ability. For example, if you aren't born to become a scientist, good school and education won't help you achieve that.
 
When I say there's a limit where good education can take you, I didn't imply that education isn't important but rather I was trying say that education can't replace innate ability. For example, if you aren't born to become a scientist, good school and education won't help you achieve that.

Hakuna kitu kama innate ability kila mtu lazima ajifunze na ku develop skills. Innate ability iko kwa samaki tu anazaliwa na kujua kuogelea hapo hapo hata hivyo skills wanatapata baadae.
 
Back
Top Bottom