nyumbamungu
JF-Expert Member
- Mar 3, 2017
- 1,033
- 895
Habari za jioni wadau, kunatetesi kuwa Mkataba kati ya Maxcom Afrika (Maxmalipo) na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani umekwisha na hawajaongezewa muda tena. Tetesi hizo zipo baada ya Jeshi la Polisi Usalama barabarani kukabidhiwa mashine za kutoza faini zinazomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, sio zile za Maxmalipo.
Tofauti na awali dereva anapopigwa faini ya barabarani alikuwa analipa kwa wakala wa Maxmalipo, lakini kwasasa haziwezi kulipia faini hizo tena. Pia mfumo wa awali uliokuwa unaendeshwa na Maxcom Africa ulikuwa unamsaidia dereva kufahamu kiwango cha malipo anachotakiwa kulipia kwa kupiga (Shot Code) mfumo saidizi, kutumia simu *152*75#
Kwasasa ukitumia mfumo saidizi kuangalia deni *152*75# inarudisha majibu gari halidaiwi, wakati deni lipo. Lakini ukisoma karatasi ya faini ina maelezo lipia tawi lolote la NMB au kwa mitandao ya simu tumia namba ya kampuni 888999.
Tunaomba Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kutoa elimu kwa umma kutokana na mabadiliko hayo, Kwani ukipiga simu Maxcom Africa kutaka ufafanuzi wa majibu wanayotoa hayana msaada kwa dereva, watakwambia uwatajie namba ya gari waangalie kiwango unachotakiwa ulipie wakitazama mfumo wao unaonesha hakuna deni. Ukweli wangekuwa wazi kwa kuwaambia wanaouliza kuwa kuna mtoza faini mwingine.