Maxence Melo: Tulipata changamoto kuhusu Sera yetu ya Faragha na haikuwa rahisi kufanya kazi na Serikali

Maxence Melo: Tulipata changamoto kuhusu Sera yetu ya Faragha na haikuwa rahisi kufanya kazi na Serikali

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mkurugenzi wa Jamiiforums leo ameongelea mchango wa dijitali kwenye demokrasia ikiwemo walipofikia na changamoto zake kwenye mjadala uliofanyika Msasani, Dar es Salaam.

Maxence Melo: Tulipata changamoto sana kuhusu Sera yetu ya Faragha lakini kwa sasa tumeshaandaa Muswada mbadala wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi na Faragha.

Ninashukuru kwamba Wizara inatoa ushirikiano mkubwa kwenye hili. Kila Mdau wetu atapata nafasi ya kushiriki kutoa maoni.

Pia Maxence amesema awali haikuwa rahisi kufanya kazi na Serikali na taasisi zake lakini sasa wanapata ushirikiano mkubwa.
AA8A1135.jpg
 
Serikali ilitaka wote tufahamike ili iwe rahisi kwao kumchukua yeyote mwenye mdomo ahahahaaa, msimamo thabiti ni heshima japo yenye uchungu.
 
Bavicha ndio huwa wanamponza boss kubwa
Btw tunaomba lirudi lile chimbo
 
Serikali ya Legendary wako?
Serikali ilitaka wote tufahamike ili iwe rahisi kwao kumchukua yeyote mwenye mdomo ahahahaaa, msimamo thabiti ni heshima japo yenye uchungu.
 
Na huku kwenye technical bench lake nako afanye Demokrasia na asiishie kuiomba kwenye media zingine bali atekeleze kwake kwa vitendo.
 
[mention]Maxence Melo [/mention] tajiri ongea nao basi warudishe lile jukwaa letu la Far Southern
 
Back
Top Bottom