Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
siku ya jumamosi ndiye namuona kama mchezaji hatari kwa Simba SC kutokana na ubora wake ndani ya uwanja, Maxi kama yupo fiti lazima atakupa mechi bora sana kuanzia nguvu hata kasi na ufanisi kwenye maeneo mengi ndani ya uwanja yameipa uhai mkubwa sana Young Africans
Mechi tatu zilizopita za Kariakoo Derby amefunga magoli matatu ambayo kwa kiasi kikubwa yaliamua mechi hizo, hivyo kama kuna mchezaji wa kwanza ambaye Simba wanapaswa kumtazama kuelekea mchezo huu basi ni Maxi Nzengeli ambaye aliwapa mechi ngumu sana kwenye eneo la mwisho pale ambapo walikutana naye
Pale Young Africans ukiacha Pacome Zouzoua, Aiz Ki, Clatous Chama na wachezaji wengine ambao wanaimbwa sana kutokana na vitu vingine vya ziada walivyo navyo miguuni mwao basi wapo wachezaji wengine ambao naona ni muhimu sana kwenye kikosi cha Miguel Gamondi, Na miongoni mwa wachezaji hao ni Maxi Nzengeli ambaye hana mambo mengi mguuni tofauti na kufanya majukumu ya msingi uwanjani
Maxi hana muda wa kucheza sana na majukwaa tofauti na mpira wake uwanjani, mpe mpira atafanya majukumu ya msingi na kama hamna mpira basi atautafuta eneo lolote lile ndani ya uwanja! One of the Best, Benchi la Ufundi la Young Africans nadhani ukiwaambia wataje majina ya wachezaji ambao hawapaswi kukosa kwenye daftari lao basi jina la Maxi Nzengeli hawawezi kuliweka pembeni
SIMPLY! Kwa sasa sio mchezaji ambaye utasikia akizungumzwa sana lakini binafsi hii naona ndio silaha ya Miguel Gamondi ndani ya uwanja, ni ngumu sana kunielewa kwa sasa lakini kama umetazama vyema mechi za Young Africans unaweza kukubaliana na mimi kwa asilimia kubwa sana! Player to Watch 👊
Let's Goo!!.