kesha fikia point of diminishing Maximo.aondoke zake watafute mwingine kwa miaka mitatu kwa ajili ya mashindano na cyo friend match.
hana jipya tena sana sana ataleta siasa tu hapa Bongo
Tatizo hapa sio Maximo, tatizo ni kuanzia viongozi wa TFF hadi wa vilabu. si TFF wala vilabu wenye vitega uchumi ambavyo vingewezesha kupatikana kwa fedha za kuendesha programmes mbalimbali kama training za makocha, viongozi wa kisasa wa mpira na ligi kama ilivyokuwa Taifa cup enzi zile. kupata vipaji vipya TFF ingeazisha mashindano mfano wa kombe la FA, zamani kulikuwa na kitu kama hicho kama sijakosea. hapa wangeruhusu vilabu hata vya kijini kabisa kushiriki, nina hakika tungepata vipaji vipya vya kutosha,, tatizo fedha na viongozi hawako craetive kupata vyanzo vya hela wote wnasubiri mechi za simba/yanga waweke viingilio vikubwa au wapate hela za wahisani na zile za FIFA kwa stahili hii kamwe huwezi kuwa na timu ya taifa imara.
Vilabu vingi havina viwanja wala majengo ya vitega uchumi,hakuna register ya wanacha, huwezi kuwa na vilabu vikubwa kama yanga/simba ambapo wanachama wanaopiga kura hawazidi 500!
vilabu kamwe havitaendelea kwa fedha za wafadhili,sbb hao wafadhili wana agenda yao ya siri wao si wajinga wapoteze hela za burebure tu, viongozi wa vilabu wanategea kuendesha maisha yao kutumia vilabu, katika mazingira kama hayo unategemea nini, hasa katika nchi ambayo viwanja vyote vya ni vya aidha serekali au CCM?
Klabu kama simba au Yanga wangeweza kabisa kuwa na majengo yao, achana na yale magofu ya kariakoo, wangejenga viwanja ili yale mapato wanayolipia gharama za uwanja pale taifa zingeingia kwao moja kwa moja, wangesini mikataba na makampuni ya nguo kutengeneza jezi/t-shrt/lesso/raba/kandambili/mikanda/skarf n.k zenye nembo yao na wangepata mamilioni ya kutosha ya kuwawezesha kuwa na academic schools za kuzalisha wachezaji na kuwauza na kupata a lot of money tatizo lilelile wako pale kwa maslahi yao sio ya klabu/taifa.
katika nchi kama hii usitegemee maajabu kwa timu ya taifa wakati vilabu ni vibovu. TFF ilitakiwa igenerate fedha za kutosha kustimulate vyama vya mikoa na sio koconcentrate dar peke yake,sidhini hata kama wana plan ya next five years to come. Hata website hawana unategemea nn hapo.
//