Mayai kutototolewa kwa kiwango mikubwa. Tatizo laweza kuwa ni Mayai au Incubator?

Mayai kutototolewa kwa kiwango mikubwa. Tatizo laweza kuwa ni Mayai au Incubator?

lingamba lidodi

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2018
Posts
964
Reaction score
1,137
Nimenunua incubator ya kutengeneza hapa ndani. Tarehe10/12/2018,niliweka Mayai tray 20 kwa Mara ya kwanza. Mwisho wa siku vimetoka vifaranga30 tu. Wajuzi nisaidieni,hapo tatizo ni Mashine au Mayai? Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kuna vitu viwili moja inawezekana mayai yako mengi hayakutokana na jogoo(infertile) pili incubator yako ina matatitizo.

Kama utahitaj ushauri au matengenezo ya incubator yako kuongeza efficiency maana hiyo itakulisha hasara ni pm tuyajenge
 
Nimenunua incubator ya kutengeneza hapa ndani. Tarehe10/12/2018,niliweka Mayai tray 20 kwa Mara ya kwanza. Mwisho wa siku vimetoka vifaranga30 tu. Wajuzi nisaidieni,hapo tatizo ni Mashine au Mayai? Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
REFER TO... inaweza kuwa mayai au incubetor
kwa upande wa mayai nikama ifuatavyo
1; yai lako unatakiwa utunze kwa muda usio zidi siku nane tangu limetagwa na kuku.
2; joto la mazingira ya kawaida inatakiwa lisizidi 35c kwani ni moja ya changamoto inayo pelekea kifaranga kufa ndani ya yai
hiii ni baada ya vimengenya vinavyo patikana ndani ya yai kuanza kufanya kazi pindi joto linapo kuwa kwenye usawa wa nyuzi 35-37 hivyo bac ili yai liwe safi kipindi cha kuhifadhi ni vizur likatunzwa kwenye mazingira ya nyuzi kati ya 18-24
3; kuna jinsi ya kulihifadhi yai lako ilikuzuia ukuaji na kufanya lisiharibike kipindi cha makusanyo
hapa lazima ujue kwa kawaida mayai yana pande mbili yaani upande ulio chongoka na upande nusu duara
4;lazima kuku awe najogoo mchakalikaji hususa kwenye kuwapanda tetea ili kuhakikisha mayai yanakuwa na mbegu xy kwa maana ya kifaranga ambacho hakijaanza kukua.

upande wa ncubetor
mimi mwenyewe ni fundi wa kuziunda ila kiukweli kosa la mafundi wengi tunatamaa ya hela katika hili unaweza kuuziwa incubetor lakini ikawa na mapungufu kama yafuatayo
1 kuto kuzalisha unyevu wa kutosha
2; kuzalisha joto lisilo na muelekeo maalum
3; kutokuwa na kifaa cha kudhibiti joto / kina kuwepo lakini hakifanyi kazi vizur
4; vipimo kutoa majibu ambayo sio sahihi
kwa kusema haya nadhani mh unaweza ukafanya uchunguzi kuanzia kwenye mayai yako mpaka kumtafuta aliye kuuzia incubetor ili akupe kitabu cha muongozo pamoja na semina fupi jinsi ya kutumia hiyo incubetor.
ASAHNTE KAMA UMENIELEWA MR
 
uliweka tray 20,ukapata vifaranga 30
maelezo yako hayajakamilika
swali 1; ni maya ya namna gani na uliyapata wapi,tatazo mtu anadhani incubator inaweza kutotoa mayayi yoyote yale,kwahiyo unabeba kokote ukiona kuna mayai
swali 2;unajua kutumia incubator,hebu tuweke picha ya hiyo incubator ,incubator ya inayobeba tray 20 sio mchezo
 
Back
Top Bottom